Design a site like this with WordPress.com
Get started

Siri Namba Moja Ya Kupata Fedha

Kwenye kitabu cha The Baron letters, mwandishi Gary Halbert alimwandikia barua mtoto wake akiwa gerezani.

Gary Halbert alikuwa mwandishi bora kabisa wa matangazo na hivyo alitumia muda wake kumshirikisha mtoto wake yale yote aliyojifunza kwenye maisha, kuanzia kuwa na afya bora, kupata nk.

Hata wewe kama ni mzazi unaweza ukawa unaandika yale uliyojifunza na kumshirikisha mtoto au watoto wako.

Mwandishi, alimshirikisha mtoto wake siri namba moja ya kupata fedha.

Mwandishi anasema kama akiulizwa ipi siri namba moja ya kupata fedha atajibu hamasa na mapenzi.

Anasema mtu anapaswa kufanya kile anachopenda kufanya, kile ambacho ana hamasika kukifanya na hapo ndipo mtu anaweza kupata fedha nyingi atakavyo.

Mwandishi Gary Halbert anasisitiza kwamba fedha ni zao la hamasa, kama mtu anapenda kuwa msanifu majengo, hapaswi kukimbilia kuuza majengo kwa sababu amesikia kuna fedha.

Kitu cha kuondoka nacho hapa, fedha zipo kule ambapo hamasa ya mtu ipo.

Hamasa na shauku ndiyo sifa inayolipa zaidi duniani. Kwenye kila unachofanya, igiza kuwa na hamasa au shauku KUBWA itakusaidia kuongeza ushawishi, kukubalika na hatimaye kufanikiwa kwenye kile unachotaka.

Hatua ya kuchukua leo; jiulize hamasa yako ipo wapi?
Ukishajua peleka nguvu zako kule ambapo hamasa ya mtu ipo.

Hamasa inalipa, fanya chochote kile kwa hamasa na shauku KUBWA utaongeza vitu vingi ambavyo ulikwa huna.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha  ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blo

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: