Design a site like this with WordPress.com
Get started

Jinsi Ya Kuongeza Kiwango Chako Cha Utambuzi

Je, unajua kiwango chako cha utambuzi?

Kabla hujaongeza kiwango chako cha utambuzi, unapaswa kwanza kujua au kupima kiwango chako cha utambuzi kikoje.

Njia ya kupima kiwango chako cha utambuzi ni kwenye kujua majira ya siku.
Hapo inakuwaje sasa?
Ni rahisi sana, kwa mfano, bila ya kuangalia saa, sema muda ni saa ngapi yaani sema saa na dakika.

Baada ya kubashiri muda na dakika, kinachofuata baada ya hapo angalia saa yako kulinganisha muda uliosema na muda halisi kwenye saa yako.

Utajuje sasa kama una utambuzi?

Ili uweze kujua kama una utambuzi, unapaswa kuwa ndani ya dakika 7 za muda halisi, kwa mfano, kama muda halisi ni saa tano na nusu, basi bila kuangalia saa muda utakaoutaja uwe kati ya saa tano na dakika 23 mpaka saa tano na dakika 37.

Na kama muda unaotaja bila ya kuangalia saa utakua umezidi au kupungua zaidi ya dakika kumi za muda halisi, utakua upo chini sana kiutambuzi na unatakiwa kuchukua hatua mara moja ya kuongeza kiwango chako cha utambuzi.

Na habari njema ni kwamba, njia ya kupandisha kiwango chako cha utambuzi ni kuacha unachofanya na kuwa na matembezi au kufanya chochote kitakachouweka mwili kwenye mwendo kama vile mazoezi.

Hatua ya kuchukua leo; kaa chini pima kiwango chako cha utambuzi kwa kufuata utaratibu ambao umejifunza leo kwenye makala hii.

Kwahiyo, ili uwe na utambuzi unapaswa kuuweka sana mwili wako katika mwendo, kwa sababu kama akili yako ikilala na wewe utalala pia.
Mchezo mzima kwenye maisha yako uko kwenye akili, akili yako ikiwa vizuri na kila eneo la maisha yako litakuwa vizuri sana.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha  ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: