Design a site like this with WordPress.com
Get started

Unaweza Kuwadanganya Mashabiki Lakini Siyo Watu Hawa

Biashara ni mchezo na wafanyakazi ndiyo wachezaji wenyewe. Na watu wa nje ni mashabiki tu.

Sasa kama biashara ni mchezo, unaweza ukawadanganya mashabiki lakini huwezi Kuwadanganya wachezaji.

Unaweza kuwadanganya mashabiki kuhusu mwenendo wa biashara yako, au familia yako, au kitu fulani kwa kuigiza kwamba mambo yanakwenda vizuri, lakini wale walio ndani wanajua kama mambo yanaenda vizuri au la.

Huwezi kuwadanganya waliopo ndani ya mchezo kwenye biashara yako, familia yako kwa sababu hata kama unaweka siri, kuna vitu wataona havipo sawa.

Hatua ya kuchukua leo; kama mambo hayako sawa, rekebisha haina haja ya kuwadanganya watu wa nje wakati mliopo ndani ya mchezo mnajionea nyie wenyewe kwamba hali siyo shwari.

Usiwadanganye mashabiki, hakuna siri itakayokaa milele, itafikia mahali kila unachoficha kitakujulikana na mashabiki.

Kumbuka, unaweza kuwadanganya mashabiki lakini huwezi kuwadanganya wachezaji. Mashabiki ni watu nje na wachezaji ndiyo wahusika mwenyewe.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha  ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: