Design a site like this with WordPress.com
Get started

Ukiwa Na Hali Hizi, Epuka Kufanya Maamuzi

Kwenye kitabu cha the Baron letters kilichoandikwa na mwandishi Gary Halbart,  anamshirikisha  mtoto  wake  makosa  ambayo  amewahi kuyafanya kwenye  maisha  yake,  na  mengi aligundua  aliyafanya  akiwa  kwenye  moja  ya  hali  hizi nne.  Hivyo  anamwambia  mtoto  wake  asifanye  maamuzi  yoyote anapojikuta  kwenye moja  ya  hali  hizo  nne;

Moja; hasira. Usifanye maamuzi ukiwa kwenye hasira, jisubirishe kufanya maamuzi pale unapokuwa na hasira juu ya kitu fulani mpaka pale hasira zitakapopoa.

Mbili; njaa. Mtu akishakuwa na njaa, anachofikiria yeye ni chakula ili ashibishe njaa yake na akishiriki kwenye maamuzi anakuwa hafikirii bali analazimisha maamuzi kwa sababu mwili unamsukuma kufanya hivyo.

Tatu; upweke. Watu wanapokuwa katika upweke, wanakuwa wanafanya maamuzi ya hisia za hofu.

Nne; uchovu. Ukiwa umechoka, usifanye maamuzi kwa sababu mwili unakua unataka kupumzika.

Hatua ya kuchukua leo, ukiwa kwenye  hali  yoyote katika  hizo  nne,  maamuzi  utakayoyafanya hayatakuwa  bora  kwako.

Badala  yake, unapogundua  upo  kwenye  hali  yoyote  katika  hizo,  fanya  kitu kitakachoufanya  mwili  uwe  na  kazi,  labda  kutembea,  kukimbia,  kuandika  au  kuongea na  wengine. Epuka  kufanya  maamuzi  kwenye  hali  hizo  nne.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha  ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: