Design a site like this with WordPress.com
Get started

Jifunze Kwa Mtu Aliyepitia Magumu Na Akafanikiwa Ndoto Yake

Tabia huwa zinatengenezwa pale tunapopitia magumu.

Katika magumu, ndiyo watu huwa wanatumia uwezo wao mkubwa uliopo ndani yao.

Na uzuri ni kwamba hakuna mtu ambaye hana changamoto yaani yeye nyumbani kwake amebandika bango mlangoni kwamba hapa hakuna matatizo.

Ulishawahi kuona nyumba ya namna hiyo? Kama hujawahi kuona, jua kwamba kila binadamu anapitia magumu yake.

Leo nataka ujifunze kupitia kwa aliyekuwa Raisi wa awamu ya 16 ya Marekani Abraham Lincoln.

Huyu ni mmoja wa watu ambao walipitia magumu sana, lakini akawa mvumilivu, hajakubali kushindwa na akapambana mpaka akaweza.

Na hii hapa ni orodha ya magumu yake aliyopitia.

Angalia maisha ya mtu huyu yalivyokuwa ya Kukatisha tamaa.

Akiwa na miaka 21 alishindwa kwenye biashara.

Akiwa na miaka 22 alishindwa kwenye uchaguzi wa uwakikishi.

Akiwa na miaka 23 alishindwa kwenye biashara ya pili.

Akiwa na miaka 25 mchumba wake alikufa.

Akiwa na miaka 26 alipata ugonjwa wa akili.

Akiwa na miaka 28 alishindwa kwenye uchaguzi wa uwakilishi.

Akiwa na miaka 30 alishindwa uchaguzi mwingine.

Akiwa na miaka 33 alishindwa tena uchaguzi mwingine.

Akiwa na miaka 38 alishindwa tena uchaguzi mwingine wa uwakilishi.

Akiwa na miaka 45 alishindwa kwenye uchaguzi wa useneta.

Akiwa na miaka 46 alishindwa kwenye uchaguzi wa makamu wa raisi.

Akiwa na miaka 49 alishimdwa tena kwenye uchaguzi wa useneta.

Akiwa na miaka 50 alichaguliwa kuwa raisi wa marekani.
Maisha yake ya kushindwa yalimfanya awe bora zaidi na kuweza kupambana mpaka akafanikiwa kuwa raisi wa marekani na kuweza kuiongoza nchi hiyo kwenye vita vya kiraia.

Hatua ya kuchukua leo; kitu cha kuondoka nacho hapa ni;

Uvumilivu unalipa sana, nenda kawe na uvumilivu kwenye maisha yako, magumu unayopitia yanakuandaa kwa ajili ya mambo makubwa zaidi.

Rafiki yangu nikupendaye, kila kitu kinachokuja kwako, huwa kinakuja kwa kusudi fulani.
Kila magumu unayopitia jiulize hili nalo limekuja kwa kusudi gani.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha  ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: