Design a site like this with WordPress.com
Get started

Kosa Ambalo Wauzaji Wengi Huwa Wanalifanya Kwenye Biashara

Unaweza kupata chochote kile unachotaka kwenye maisha yako, kama utaweza kuuza zaidi. Ni kweli hilo halina ubishi, mauzo ndiyo kila kitu kwenye biashara na maisha kiujumla.

Mauzo ndiyo moyo wa biashara, ambapo yanasukuma damu ya biashara ambayo ni fedha. Bila mauzo hakuna fedha kwenye biashara, na bila fedha hakuna biashara. Unaona hapo mauzo yalivyokuwa muhimu?

Kosa ambalo wauzaji wengi wamekuwa wanalifanya ni kuwasahau wateja. Kwa mfano, kama umewahi kununua kitu kimoja sehemu tofauti zaidi ya 30 basi ujue hapo kuna shida kwa muuzaji.

Kwa mfano, mwandishi wa kitabu cha How I Raised Myself From Failure to Success in Selling anasema aliwahi kununua magari 30 kwa wauzaji tofauti, yaani katika magari hayo 30, kila gari amenunua kwa muuzaji wake. Hapo ndiyo akagundua kwamba wauzaji wengi wanafanya makosa ya kuwasahau wateja wao.

Laiti kama muuzaji wa kwanza angemfuatilia mteja wake angeweza kumuuzia gari la pili.

Leo nakwenda kukushirikisha kauli mbiu ya kampuni moja kubwa ya magari iitwayo Chevrolet Motor Company inayosema, KAMWE USIMSAHAU MTEJA, KAMWE USIRUHUSU MTEJA AKUSAHAU.

Wewe kama muuzaji usiruhusu mteja AKUSAHAU, endelea kuwasiliana na mteja baada ya kumuuzia kitu au huduma fulani hii itakusaidia kumrudisha tena mteja kuja kununua kwako pale anapokuwa na uhitaji.

Unaweza ukaongeza mauzo leo kwa kuwakumbuka wateja wako wote uliowahi kuwauzia kwa kuwapigia simu au kuwatembelea.

Biashara yako isiishie tu pale unapomuuzia mteja, bali endelezeni mahusiano, kama hatorudi tena kununua atawaambia watu wake wa karibu, ndugu, jamaa au marafiki.

Hata kwenye mahusiano ya kawaida, kama kuna mtu unahusiana naye, usiruhusu AKUSAHAU.

Kumbuka, kile unachokipa muda, ndiyo kinakupa matokeo mazuri pia. Ukiwathamini wateja wako nao watakuthamini pia.

Binadamu tunayo kawaida ya kulipa fadhila, hivyo unatengeneza deni juu ya kitu fulani watu wanakuwa wanaona ni vema kulipa deni hilo kama sehemu ya kurudisha fadhila.

Hatua ya kuchukua leo; KAMWE USIMSAHAU MTEJA, KAMWE USIRUHUSU MTEJA AKUSAHAU.

Sina uhakika kama itakufaa lakini tumia kauli hii kwenye biashara yako na usiruhusu mteja asaulike na wala kusahau kuhusu biashara yako.

Endelea kuwafuatilia hata baada ya kufanya manunuzi. Jua wanaendeleaje na kile ambacho wamenunua. Hii itakusaidia kuongeza mauzo kwenye biashara yako, utajitofautisha na wafanyabiashara wengine.

Habari njema ni kwamba, ninatoa huduma ya kukusaidia kuongeza mauzo kwenye biashara yako, Kama unahitaji kupata fedha zaidi kupitia mauzo, wasiliana nami kitakusaidia mbinu za masoko na mauzo.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha  ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: