Ukitaka Kuuza Sana Gusa Hisia Hizi Za Mteja Wako

Watu huwa wanaongozwa na hisia kuu mbili.Moja hisia ya kupata na mbili ni hisia ya kupoteza. Ukitaka kuuza, hakikisha unagusa hisia za wateja wako. Hisia kama za maumivu, kupoteza, matumaini, hofu nk. Unapaswa kujua kwamba, watu hawafanyi manunuzi kwa njia ya fikra bali hisia. Unagusa hisia za wateja wako pale biashara yako inapokuwa halisi na …

Usiwe Na Mtazamo Huu Kuhusu Mteja Unayefanya Naye Biashara au Kazi

Ni imani yangu kwamba ,kila mtu anauza na kila mtu ana kitu anauza. Kama umeajiriwa basi unauza ujuzi na muda wako. Kwa namna yoyote ile kila mtu ana kitu anauza, bila kuuza maana yake hauna maisha. Na kazi ya mauzo ni kazi inayokuhusisha na watu kifupi unaweza kusema ni mteja. Usiwe na mtazamo hasi kuhusu …

Sina Uhakika Kama Itakufaa Lakini Kuna Kitu Kimoja Hapa Napenda Ujifunze

Rafiki yangu, sina uhakika kama itakufaa lakini jifunze kutokujali wengine wanakuchukuliaje. Watu wengine huwa wanakosa raha pale wanapokuwa wanafikiria wengine watawachukuliaje. Kwenye maisha yako, usijali kuhusu wengine watakuchukuliaje bali wewe ishi vile utakavyo kikubwa tu usivunje sheria za asili na nchi. Ukijali sana wengine watakuchukuliaje utashindwa kufanya kazi yako na kuishi maisha yako. Nipende tu …

Hakuna Njia Rahisi Ya Kupoteza Hela Kama Hii

Kuigiza una hela. Watu wengi wanaopoteza fedha sana ni wale wanaotaka kuonekana au kuigiza kama wana hela au kitu fulani. Kumbuka maisha ni maigizo , kadiri unavyoigiza una hela lazima kuna gharama utaingia ili uonekane una hela. Utaigiza uko na kitu fulani, utaigiza uko mazingira fulani ambayo unataka watu wengine wakuone kama vile una hela …

Wape Watu Hawa Kipaumbele

Ni familia yako. Pata picha ukiumwa au ukipata tatizo ni nani anakua yuko tayari pamoja na wewe? Ni familia yako. Ukiumwa familia yako ndiyo inayopambana kuhakikisha unakua bora lakini watu wa nje hawatakua na habari na wewe. Kwa mfano, mke au mume ukiumwa atakayekuhangaikia ni mke au mume wako lakini siyo mchepuko wako. Hapo unapata …

Changamoto Zote Kwenye Biashara Zinatatuliwa Na Kitu Hiki Kimoja

Ni mauzo tu. Mauzo ndiyo yanayotatua changamoto kwenye biashara. Kama biashara haina mauzo lazima itakua na changamoto nyingi. Kwa sababu mauzo ndiyo yanaleta fedha kwenye biashara. Na fedha ikiwepo kwenye biashara, biashara lazima itaenda vizuri. Fedha itakusaidia kujilipa, kulipa gharama za biashara, kuajiri watu bora, kulipa kodi na gharama zingine ambazo fedha inaweza kutatua. Mauzo …

Msingi Bora Wa Maisha Na Mafanikio

Msingi bora wa maisha na mafanikio ni USIFANYE KITU UNACHOKICHUKIA. Watu ambao wanafanya vitu wasivyovipenda huwa hawafanikiwi, wanaishia kuwa na maisha ya kulalamika na manung'uniko. Baraka haiwezi kuja kwa njia ya manung'uniko hata siku moja. Baraka inakuja pale unapokuwa unajisikia furaha unapotoa mchango wako kwa wengine. Kwa sababu baraka inakuja kwa kufanya kitu na ukifanya …

Kitu Kimoja Muhimu Sana Cha Kujifunza Kuhusu Mauzo Kutoka Kwa Aliyekuwa Muuzaji Bora Wa Magari Duniani

Joe Girard alikuwa ni muuzaji bora wa magari na alifanikiwa kuingia kwenye kitabu cha maajabu ya dunia GUINESS kwa sababu ya kuuza sana. Ni muuzaji ambaye hajawahi kutokea duniani, na kwa kuwa maisha ya binadamu ni mauzo nasi pia tunatakiwa kujifunza mbinu za mauzo. Kila mtu ni muuzaji, kila mtu ana kitu anauza. Kwenye kitabu …

Kama Hupati Matokeo Kuna Kitu Hukifanyi

Hakuna watu ambao wana maigizo mengi kama binadamu. Ni wazuri wa kutengeneza sababu za kile ambacho wao wanaona zitawalinda. Na kama mtu kitu ana kitaka kweli atakifanya na matokeo yataonekana. Na kama mtu kitu hakitaki hatokifanya na ataanza kutafuta sababu. Maisha ni kuuza kile unachokiamini, sasa kama wewe unajidanganya kwa sababu unafikiri utapata matokeo gani? …

Umejitoa Kwa Lipi Haswa?

Utaishia kupata matokeo ya kawaida kama hujajitoa haswa kupata kile unachotaka. Binadamu ni watu wazuri sana kufanya pale wanapokuwa wanasimamiwa au wanapokuwa wamepewa namba au lengo la kufanyia kazi. Unaweza ukajiona umefikia ukomo na ukaweka nukta lakini nakuhakikishia ukiweza kujisukuma na ukapata mtu anayekusimamia utashangaa pale ulipoweka nukta panabadilika na kuwa mkato. Usiishi bila kuwa …

Design a site like this with WordPress.com
Get started