Hakuna watu ambao wana maigizo mengi kama binadamu. Ni wazuri wa kutengeneza sababu za kile ambacho wao wanaona zitawalinda.
Na kama mtu kitu ana kitaka kweli atakifanya na matokeo yataonekana. Na kama mtu kitu hakitaki hatokifanya na ataanza kutafuta sababu.
Maisha ni kuuza kile unachokiamini, sasa kama wewe unajidanganya kwa sababu unafikiri utapata matokeo gani?
Kama hupati matokeo basi kuna kitu hukifanyi. Kwa mfano, umepanda mahindi halafu unataka uvune mtama.
Ukitaka upate matokeo kweli, kaa kwenye mchakato sahihi, fanya kile unachopaswa kufanya kweli. Usiishi katika mazoa na kutegemea mambo yatatokea pasipo wewe kubadilika.
Kama unataka kuboresha kitu lazima ufanye kitu. Huwezi kuboresha kitu ambacho hakijafanyika.
Usijipe visingizio, weka silaha zote kwenye kazi na utaona matokeo hatakama siyo makubwa.
Usiishie tu kujifunza bali fanyia kazi yale unayojifunza. Usilalamike hali ngumu, je, kama hali ngumu wewe umechukua hatua gani? Unawasemea watu hawana hela je, umeona maisha yao yakisimama? Wameacha kula? Kuvaa?
Hatua ya kuchukua leo; Fanya kazi yako na matokeo yataonekana.
Kama hupati matokeo basi jua kuna kitu hukifanyi, jiulize nini unachotakiwa kufanya na hukifanyi ili upate matokeo mazuri.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog