Ni familia yako.
Pata picha ukiumwa au ukipata tatizo ni nani anakua yuko tayari pamoja na wewe? Ni familia yako.
Ukiumwa familia yako ndiyo inayopambana kuhakikisha unakua bora lakini watu wa nje hawatakua na habari na wewe.
Kwa mfano, mke au mume ukiumwa atakayekuhangaikia ni mke au mume wako lakini siyo mchepuko wako.
Hapo unapata picha kwamba, weka nguvu kubwa katika kujenga mahusiano imara katika familia yako.
Usipoteze nguvu kuhangaika na mahusiano ya hovyo ambayo yanakuingiza kwenye hasara.
Hakikisha familia yako inakua bora na wape misingi mizuri sana itakayowaongoza.
Usitoe siri za familia kwa watu ambao siyo muhimu kujua.
Linda familia yako kwa gharama yoyote ile. Pata picha kila siku unatokea nyumbani na unarudia nyumbani ni sehemu pekee unayopaswa kuiheshimu sana kwenye maisha yako.
Hatua ya kuchukua leo; Ipe kipaumbele familia yako na achana kwani familia yako ndiyo sehemu ambayo unaishi.
Familia yako ni sehemu ya pili ya mwili wako. Hivyo unapokuwa tofauti, familia yako itakua bega kwa bega na wewe ukilinganisha na watu wengine.
Kipaumbele cha kwanza kwenye maisha yako ni familia yako.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog