Kuigiza una hela.
Watu wengi wanaopoteza fedha sana ni wale wanaotaka kuonekana au kuigiza kama wana hela au kitu fulani.
Kumbuka maisha ni maigizo , kadiri unavyoigiza una hela lazima kuna gharama utaingia ili uonekane una hela.
Utaigiza uko na kitu fulani, utaigiza uko mazingira fulani ambayo unataka watu wengine wakuone kama vile una hela na vitu vyote hivyo vitakuingiza gharama.
Hivyo unajikuta unapoteza hela zaidi kuliko kuwa kawaida.
Unapoteza hela kuwafurahisha watu wasiojali. Wataki mwingine unatumia hela ambazo huna yaani kukopa kutaka kuwafurahisha watu wasiojali.
Usifanye kitu ili watu wakuone, wewe igiza unavyoweza lakini kumbuka unayeumia ni wewe.
Mwenye hela huwa hataki kuonekana kama ana hela ila hela zenyewe zinamfanya aonekane ana hela bila hata kutumia nguvu kubwa.
Ya nini kutumia gharama kubwa kuigiza kama una hela halafu huna hela?
Usiogope kuishi maisha yako, usiigize maisha yako maana utajipoteza. Kumbuka kitu kimoja kwamba wewe ndiyo mkurugenzi wa maisha yako.
Maisha ya kuigiza yana gharama kubwa kuliko maisha ya uhalisia. Ishi uhalisia wako na utaokoa gharama zisizokuwa na msingi.
Hatua ya kuchukua leo; Usiigize maisha kuonekana una hela hata siku moja halafu huna hela ndiyo utapoteza hela nyingi kuliko maelezo kwa sababu maisha ya kuigiza yana gharama kubwa.
Kitu kimoja cha mwisho rafiki yangu, hakuna njia rahisi ya kupoteza hela kama kuigiza una hela.
Ishi uhalisia wako na utaweza kuokoa gharama kubwa.
Hakuna watu wanaojali maigizo yako, ni bora kuishi uhalisia wako tu. Kila mtu yuko bize na maisha yake unaweza kuona unataka uonekane kumbe hakuna hata mwenyewe muda wa kuangalia maigizo yako kila mtu ana kitu ambacho kinamkosesha usingizi lakini siyo maigizo yako.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog