Watu huwa wanaongozwa na hisia kuu mbili.
Moja hisia ya kupata na mbili ni hisia ya kupoteza.
Ukitaka kuuza, hakikisha unagusa hisia za wateja wako. Hisia kama za maumivu, kupoteza, matumaini, hofu nk.
Unapaswa kujua kwamba, watu hawafanyi manunuzi kwa njia ya fikra bali hisia.
Unagusa hisia za wateja wako pale biashara yako inapokuwa halisi na inapokuwa na utu. Pale mteja anapoona anathaminiwa kama mtu siyo tu kwa ajili ya kuumizwa na kuuziwa.
Pale mteja anapoona anachukuliwa kama rafiki na hapo anaona ni wajibu kwake kuilipa biashara hiyo kwa sababu imemjali.
Kifupi ukitaka kuuza sana angalia hisia za watu kuliko fikra. Hisia zinazidi fikra.
Ongea na mioyo ya watu kabla hujaongea na akili za wateja wako.
Hatua ya kuchukua leo; hisia ndiyo zinawafanya watu kuchukua hatua hivyo ukitaka kuuza cheza na hisia za watu na siyo fikra.
Watu hawanunui kwa kutumia fikra, bali wananunua kwa kutumia hisia.
Hisia ndiyo zinawafanya watu wengi kuchukua hatua, wakati fikra zinawafanya watu kufikia hitimisho la kitu fulani.
Hivyo basi, kama unataka kuwauzia wateja wako, gusa hisia zao.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog