Utaishia kupata matokeo ya kawaida kama hujajitoa haswa kupata kile unachotaka.
Binadamu ni watu wazuri sana kufanya pale wanapokuwa wanasimamiwa au wanapokuwa wamepewa namba au lengo la kufanyia kazi.
Unaweza ukajiona umefikia ukomo na ukaweka nukta lakini nakuhakikishia ukiweza kujisukuma na ukapata mtu anayekusimamia utashangaa pale ulipoweka nukta panabadilika na kuwa mkato.
Usiishi bila kuwa na lengo kwenye kila eneo la maisha yako. Jiwekee malengo halafu kila siku kuwa na msimamo kwenye malengo yako.
Jisukume kadiri uwezavyo kwenda viwango vya juu. Jiambie kabisa hapo ulipo sasa siyo “levo” yako unatakiwa kwenye viwango vya juu zaidi.
Jifunze kujipandisha thamani kwa kufanya vitu vyenye viwango. Wafanye watu wakushangae kwa yale unayoyafanya, yaani unakuwa ni mtu ambaye hujazoeleka katika utendaji yaani wewe kila siku unakua, maboresho kila siku.
Umejitoa kwa lipi haswa? Kuwa na kitu ambacho unakipigania, unakifikiria muda wote, kitu ambacho kinakunyima usingizi.
Usipojitoa kwa lolote kwenye maisha yako, utapotea kama vile mshumaa unavyopotea kwenye upepo.
Ishi kwa namba, ishi kwa lengo usiishi tu ilimradi, jiwekee namba au lengo unalotakiwa kufanyia kazi kwa siku, wiki, mwezi. Kisha jisukume kupata namba unayotaka au kufikia lengo lako.
Maisha yanakupa mrejesho wa kile unachofanya. Kama umejitoa kweli, utapata matokeo mazuri na kama unazingua utapata matokeo yanayozingua kweli.
Hatua ya kuchukua leo; jiwekee lengo au namba unayofanyia kazi kwenye kila eneo la maisha yako.
Kwa mfano, jiwekee namba ya mauzo ya wiki, siku na jisukume kupata namba hiyo.
Usiishi kwa bahati, sababisha matokeo mazuri unayotaka kuyaona kwenye maisha yako na yatakuja kweli. Weka kazi kweli, jitume kiasi kwamba hutokuja kujilaumu kwa kujiambia laiti ningelijua.
Jitoe sasa, jitoe kafara kwenye kile unachotaka kwenye maisha yako na utakipata kweli.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog