Joe Girard alikuwa ni muuzaji bora wa magari na alifanikiwa kuingia kwenye kitabu cha maajabu ya dunia GUINESS kwa sababu ya kuuza sana.
Ni muuzaji ambaye hajawahi kutokea duniani, na kwa kuwa maisha ya binadamu ni mauzo nasi pia tunatakiwa kujifunza mbinu za mauzo.
Kila mtu ni muuzaji, kila mtu ana kitu anauza.
Kwenye kitabu chake cha jinsi ya kuuza chochote kwa mtu yeyote ameshirikisha mbinu nyingi za mauzo ambazo yeye alizitumia na kuingia kwenye kitabu cha maajabu ya dunia.
Joe Girard anasema usisubiri wateja waje, watafute wateja ndiyo wakutafute.
Umeelewa hapo rafiki yangu? Rudia tena sentensi.
Usisubiri wateja waje, watafute wateja ndiyo wakutafute.
Hii ina maana kwamba lazima watu waijue biashara yako, yaani uitangaze na watu wajue unafanya nini. Kifupi hapo ni kufanya masoko ili watu wajue unauza nini na siku wakiwa na uhitaji wajue wanapata kwako.
Fanya masoko kisha fanya mauzo.
Kwa mfano, Joe Girard anasema kilichokuwa kinamtofautisha yeye na wauzaji wengine ni kutosubiri wateja waje, bali yeye kuwatafuta wateja.
Aliwatafuta wateja ambao hata hawajui kwa kuwapigia simu baada ya kutafuta kitabu cha namba za simu huku akiwauliza kuhusu uhitaji wao wa magari.
Ukishajua nini unauza na ukawajua wateja wako ni watu wa aina gani, kawatafute kule walipo na siyo kusubiri mpaka waje unakouzia.
Hatua ya kuchukua leo; usisubiri wateja waje, watafute wateja ndiyo wakutafute.
Ondoka na sentensi hii moja na kaifanyie kazi, fanya masoko kisha fanya mauzo.
Nenda kawe watofauti kidogo leo, wenzako wakiwa wanasubiri wateja waje, wewe ukiwafuata na kuwapigia simu utauza zaidi ya wengine.
Jaribu moja na kisha utaniambia matokeo mazuri utakayopata kwenye mauzo leo.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog