Ni mauzo tu. Mauzo ndiyo yanayotatua changamoto kwenye biashara. Kama biashara haina mauzo lazima itakua na changamoto nyingi. Kwa sababu mauzo ndiyo yanaleta fedha kwenye biashara.
Na fedha ikiwepo kwenye biashara, biashara lazima itaenda vizuri. Fedha itakusaidia kujilipa, kulipa gharama za biashara, kuajiri watu bora, kulipa kodi na gharama zingine ambazo fedha inaweza kutatua.
Mauzo yakiwa vizuri yanatatua changamoto za biashara. Ukiona watu wanalalamika hali ngumu kwenye biashara basi ujue ugumu huo unaanzia kwenye eneo la mauzo.
Sasa ni kifanyike?
Ukiona hali ngumu kwenye biashara, fanya yafuatayo.
Moja, fanya masoko kwenye biashara yako. Hakikisha watu wanajua kile unachofanya kwenye biashara yako.
Wale watu ambao wanahusina na biashara yako basi wanatakiwa kujua wewe unafanya nini ili pale watakapokuwa na uhitaji watakuja kwako.
Unapaswa utembee, nenda kawatafute wateja wapya, usikae na kusubiri mteja, andaa timu ya masoko itakayokusaidia kufanya kazi.
Ukifanya masoko sasa watu watakua wanaijua biashara yako lakini unakuwa bado hujakamilisha uhai wa biashara yako ambayo ni mauzo.
Yaani fanya yote kwenye biashara lakini mauzo ndiyo mpango mzima wa biashara. Usipofanya mauzo maana yake ni dalili mbaya kwenye biashara yako.
Usipofanya mauzo maana yake hakuna fedha inayoingia na kama hakuna fedha biashara itajiendeshaje?
Jitahidi sana kujisukuma zaidi katika eneo la masoko na mauzo.
Usifanye uzembe wala uvivu kwenye hili, jitoe kweli kweli kwenye mauzo. Kama hali ni mbaya kwenye biashara yako, amka na kupiga simu kwa wateja, tafuta wateja wapya kila siku, watembelee wateja wako na itakusaidia kuongeza mauzo.
Hatua ya kuchukua leo; Jiwekee namba ya mauzo ambayo utaifanya kwa wiki.
Baada ya kuwa na namba ya wiki, igawe kwa siku utapaswa kuuza mauzo kiasi gani.
Akili yako muda wote iwaze namna ya kuongeza mauzo. Ukishakuwa na namba ya mauzo utajisukuma. Kuwa kabisa na mwongozo wa mauzo unaokuongoza kila siku na uwe na msimamo huo.
Mteja kununua kwako mara moja ni hasara, watafute wateja wote wale ambao tayari walishawahi kununua kutoka kwako na waambie juu ya bidhaa mpya, msalimie na muulize kile ulichowahi kumuuzia kilifanyaje kazi?
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog