Msingi bora wa maisha na mafanikio ni USIFANYE KITU UNACHOKICHUKIA.
Watu ambao wanafanya vitu wasivyovipenda huwa hawafanikiwi, wanaishia kuwa na maisha ya kulalamika na manung’uniko.
Baraka haiwezi kuja kwa njia ya manung’uniko hata siku moja. Baraka inakuja pale unapokuwa unajisikia furaha unapotoa mchango wako kwa wengine. Kwa sababu baraka inakuja kwa kufanya kitu na ukifanya kitu kwa njia ya kulalamika utafanikiwaje?
Fanya unachopenda, penda unachofanya huu ndiyo msingi wa maisha bora na ya mafanikio.
Kama kuna kitu hutaki au hupendi kufanya usifanye muda wako ni mchache na wa thamani, usiupoteze kwa mambo yasiyo muhimu kwako.
Hatua ya kuchukua leo; fanya unachopenda, penda unachofanya.
Hauko hapa duniani kumridhisha kila mtu, uko duniani kujiridhisha wewe mwenyewe. Usiyapoteze maisha yako kwa kuhangaika kufanya vitu ambavyo huvipendi. Fanya vile unavyopenda na ishi utakavyo wewe kikubwa usivunje sheria za asili, nchi na misingi ya maadili.
Kuwa wewe, usiwe kama wengine.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog