Design a site like this with WordPress.com
Get started

Mpe Mteja Uhakika Huu Hapa

Kwenye biashara au huduma yoyote ile unayotoa, unatakiwa kumpatia mteja  uhakika  wa  kile  unachomuuzia.

Mfanye  ajisikie  kwamba  amepata suluhisho  na  siyo  kupoteza  fedha  zake.

Siku  zote kutoa  fedha  kunauma,  kwa sababu  unapotoa  fedha  na  kulipia  kitu,  maana  yake  huna  tena  fedha  hizo  kwa matumizi  mengine. 

Jua  mteja  wako  ana  matumizi  mengine  ya  fedha  zake, hivyo  lazima  umpe  uhakika  kwamba  atakuwa  hajafanya  makosa  kununua  kile unachouza.

Na  hata  kama  atapata  changamoto,  upo  tayari  kumsaidia  na  siyo kwamba  anakuwa  amepoteza  fedha  zake na  hajatatua  tatizo  lake.

Hatua ya kuchukua leo; Mpe mteja uhakika wa kile unachomuuzia na mfuatilie baada ya kumpatia huduma uliyompatia je, imemsaidia au la.

Mteja anaporidhika na huduma bora unayotoa ndiyo inakuwa maana ya biashara.
Kama unauza ili upate tu fedha siyo sahihi, lengo ni kumsaidia mteja kupata suluhisho kadiri ya huduma unayotoa.
Leo nenda katoe huduma bora kwa mteja wako.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha  ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: