Design a site like this with WordPress.com
Get started

Kitu Pekee Kitakachokuwezesha Kuendelea Mbele

Kuna wakati unachoka na unaona ni sahihi kwako kuishia hapo ulipofika.

Safari  ya  kupata  kile  unachotaka  kwenye  maisha  yako  haitakuwa  rahisi,  dunia haitakuachia  kirahisi ufanye  kila  unachotaka. 

Utakutana  na  vikwazo,  changamoto  na magumu mbalimbali.  Kuna  wakati utajiona  kama  umekosea  kila  ulichokuwa  unafanya.

Utafikia  hatua  ya  kukata  tamaa  na  kuona  haina  haja  ya  kuendelea  tena.

Kitu  pekee  kitakachokuwezesha  kuendelea  unapofika  kwenye  hali  kama  hii ni matumaini uliyoyatengeneza  kwenye  maisha  yako.

Kadiri unavyokuwa  na  matumaini makubwa  kwenye  kile  unachotaka  na  kwako  binafsi,  ndivyo  unavyopata  hamasa  ya kuendelea  zaidi hata  kama  mambo  ni magumu.

Wale  wanaokutana  na  magumu  sana  lakini bado  wanaendelea  siyo  kwamba  ni mashujaa  zaidi au  wana  nguvu  zaidi,  bali  wana  matumaini

Hatua ya kuchukua leo; tengeneza matumaini pale unapojikutana katika hali ya mkwamo fulani.

Siku zote mambo mazuri huwa yanakuwa mwishoni. Usikubali kukata tamaa, safari ya mafanikio makubwa iko mwishoni, endelea kukaa kwenye mchakato sahihi na matokeo mazuri unayotaka kuyaona kwenye maisha yako yatakuja yenyewe baadaye.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha  ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: