Design a site like this with WordPress.com
Get started

Hiki Ndiyo Kinaweza Kukutofautisha Na Wengine Kwenye Biashara, Kazi Au Kile Unachofanya

Kinachoweza kukutofautisha na wengine wote ambao mnafanya biashara zinazofanana, kazi au huduma zinazoendana ni utoaji wa huduma bora sana kwa wateja.

Kumbuka yoyote yule unayempatia huduma ni mteja wako. Jihoji tu, kuanzia kwenye biashara, kazi, mahusiano je, huduma ninayotoa hii kwa mteja wangu anaweza kuipata sehemu nyingine? Kama anaweza kuipata je, mimi natoaje huduma bora kiasi kwamba mteja asifikirie kwenda sehemu nyingine?

Mteja ndiyo anayeleta fedha kwenye biashara yako au huduma unayotoa. Mfanye mteja ajisikie wa kipekee kufanya biashara na wewe.

Mpatie huduma bora ambazo hajawahi kupata pengine na mfanye akienda kununua sehemu nyingine ajisikie kuna kitu anakosa na hivyo anashawishika kurudi kununua kwako.

Hatua ya kuchukua leo; jua tatizo la mteja wako kwenye kile unachofanya na kisha msaidie kutatua changamoto kadiri biashara yako.

Jali sana kuhusu biashara yako na wateja wako. Nenda hatua ya ziada katika kutoa huduma bora kabisa kwa wateja wako.

Kwahiyo, mfanye mteja ajisikie wa kipekee kufanya biashara na wewe kwa kutoa huduma bora sana ambazo hawezi kuzipata sehemu nyingine yoyote ile ila kwako tu.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha  ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: