Design a site like this with WordPress.com
Get started

Usitawanye Nguvu Zako

Rafiki, jihusishe na kitu kimoja pekee na komaa na kitu hicho mpaka utakapofanikiwa au pale uzoefu wako unapokuonesha kwamba ni wakati wa kuachana nacho.

Kwa mfano, kugonga nyundo kwenye msumari mmoja kwa kurudia rudia kunafanya msumari huo uingie ndani.

Pale ambapo umakini wa mtu unawekwa kwenye kitu kimoja, akili yake inakuwa inamletea njia za kuboresha ambazo asingeziona kama akili yake ilikuwa imezama kwenye vitu vingine vya vingi kwa wakati mmoja.

Akili yako inachoshwa na mengi kwa sababu ya kukosa utulivu. Unahangaika na mambo mengi ambayo yanamaliza nguvu zako.

Hatua ya kuchukua leo; kuwa na utulivu wa akili yako, usitawanye nguvu zako kwenye vitu vingi, tulia na vitu vichache vyenye tija kwako.

Kufanya vitu vingi visivyokuwa na maana kwako ni kutawanya nguvu zako. Elekeza nguvu zako kwenye vitu vichache na vinavyolipa.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha  ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: