Design a site like this with WordPress.com
Get started

Usiwe Na Wasiwasi Na Kitu Hiki Hapa

Kabla hatujafanya kitu chochote kile, ndani ya nafsi zetu huwa kuna sauti tunazisikia. Wakati mwingine nafsi zetu zinatuambia hapa tunaweza au hatuwezi.

Kinachowazuia wengi kufanikiwa ni kuwa na wasiwasi juu ya nafsi zao wenyewe.
Mtu anataka ushindi wa kitu fulani, lakini hajiamini kabisa kama atashinda, kimdomo anasema anataka kitu fulani lakini nafsi haimaanishi.

Kwa sababu walijaribu na kushindwa huko nyuma, hilo linakuwa linawapa wasiwasi na wanahofia kujaribu tena sasa.

Pia, kwa kuwa kuna wengine wamejaribu na wakashindwa, wanaona nao watashindwa wakijaribu.

Ili kufanikiwa usiwe na wasiwasi kabisa na nafsi yako, jiamini kwamba unaweza kufanya zaidi leo kuliko ulivyofanya jana.

Ni rahisi kuangalia nyuma na kuona sehemu ambayo ulikosea . Kama unaangalia nyuma ili kuona ni jinsi gani unaweza kuwa bora zaidi hapo sawa.

Hatua ya kuchukua leo; usipoteze muda wako kujiona kama huwezi. Usiwe na wasiwasi juu ya nafsi yako.
Jiamini na utaweza kufanikiwa kwenye kile unachotaka kwenye maisha yako.

Kumbuka majibu uliyopata zamani yanatokana na uzoefu wako wa zamani. Kama mambo hayatakwenda kama ulivyopanga tumia uzoefu wako wa sasa kuboresha zaidi.

Ondoka na sentensi hii kutoka kwa Samuel Johnson, kujiamini wewe mwenyewe ndiyo hitaji la kwanza la mafanikio.
Je, unajiamini kweli kwamba utafanikiwa bila shaka yoyote ile?

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha  ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: