Design a site like this with WordPress.com
Get started

Anzia Mahali Fulani

Kwenye maisha ili upate uzoefu wa kitu chochote kile, unapaswa kuanzia mahali fulani ili upate uzoefu.

Ukienda sehemu wanakuhitaji utoe uzoefu wako juu ya kile unachofanya, hutakiwi kubaki unatoa macho tu, bali unatoa uzoefu wako kwa kile ulichowahi kufanya.

Maisha siyo visingizio visivyokuwa na maana, bali ni kuonesha matokeo ya kile unachofanya au ulichofanya.

Ili uzoefu usiwe tatizo kwako unatakiwa kuanzia sehemu fulani kwa kuanza kufanya kitu chochote kile ambacho kinahusiana na kazi, biashara au kile unachofanya.

Kuna wakati hutakiwi kuangalia tu hela, bali angalia uzoefu utakaopata hata na utakusaidiaje baadaye kupata fedha zaidi.

Na ukipata nafasi ya kufanya ingia mzima, yaani go all in, fanya kwa uwezo wako wote wa hali ya juu, toa thamani kubwa ambayo mtu mwingine hawezi kufanya.

Wako watu wanapata nafasi ya kufanya kitu, lakini wanafanya kazi za hovyo, wakijiambia wanazugazuga tu hapa na kupotea muda huku wakisubiria ramami nyingine.

Kumbuka huwezi kupata kitu cha kufanya kizuri sana kama hicho ulichofanya umeshindwa kukifanya kwa ubora. Anza kufanya vizuri kwa kile ulichonacho hata ukipata kingine utakifanya kwa ubora wa hali ya juu sana.

Hatua ya kuchukua leo; usidharau kufanya vitu vidogo ambavyo vinakupa uzoefu juu ya kitu fulani.

Anzia mahali fulani ili upate uzoefu fulani.

Kumbuka hakuna juhudi yoyote utakayoweka na ikapotoea bure, kila unachofanya kama ni kitu sahihi lazima kitakuja kukulipa. Kazi yako kubwa ni kuendelea kubaki kwenye mchakato sahihi.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha  ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: