Design a site like this with WordPress.com
Get started

Watu Wengi Wamekosa Kitu Hiki Kwenye Maisha Yao

Leo asubuhi katika kipindi cha Billionaires in training, nimejifunza kitu kimoja kwamba watu wengi hawafanikiwi kwa sababu ya kukosa ustaarabu wa hali juu.

Ni watu wachache sana katika jamii yetu ambayo wana ustaarabu wa hali ya juu, watu wamezoea kufanya kitu mpaka waambie kufanya.

Ni kitu cha ajabu sana kwamba mtu anajua wajibu wake lakini hafanyi mpaka akumbushwe.

Watu wakipewa kazi hawafanyi kwa ajili yao, bali wanafanya kama vile wanawafanyia wengine. Kitu cha kujifunza kwenye maisha yako, uwe umejiajiri au umeajiriwa kazi yako ni ndiyo utambulisho wako na humfanyii mtu mwingine kazi bali unajifanyia wewe mwenyewe kazi.

Mtu anatakiwa kujifanyia tathmini binafsi, lakini hafanyi na kutokufanya maana yake ni kukosa ustaarabu wa hali ya juu.

Ifikie mahali uwe una kiwango cha ustaarabu wa hali ya juu, ufanye vitu vyako bila kukumbushwa na kutimiza ratiba yako kama unavyopaswa kufanya.

Usisubiri kusukumwa ndiyo ufanye, na kwa mtu ambaye ana kiwango cha ustaarabu anakuwa na uaminifu mkubwa sana kwake mwenyewe na hata kwa wengine.

Hatua ya kuchukua leo; kuwa na kiwango cha ustaarabu wa hali ya juu kwa kufanya kile unachopaswa kufanya bila kukumbushwa.

Jifunze kutoka kwa jua, huwa linawaka bila hata kuambiwa, jifunze kutoka kwa miti ya miembe, ikifika muda wake wa kutoa matunda, inatoa matunda bila hata kuambiwa.

Iweje wewe binadamu uliyebarikiwa kuliko viumbe vyote hapa duniani ndiyo unakuwa unazingua? Kuwa mstaarabu wa viwango vya juu, jua una daiwa na lipa deni na usisubiri mpaka kukumbushwa.

Una vitu vingi unavyotakiwa kukamilisha vikamilishe bila kuambiwa na huo ndiyo ustaarabu wa hali ya juu. Unajua unatakiwa kuweka akiba, kuwekeza lakini hufanyi hivyo huko ni kukosa kiwango cha ustaarabu wa hali juu.

Jenga tabia ya kuwa na ustaarabu wa hali ya juu na utafanikiwa sana kwenye maisha yako. Jua unatakiwa kufanya nini na fanya. Hakuna mtu ambaye atakuwa anakufuatilia kila siku kwenye mambo yako muhimu, unatakiwa kujifuatilia mwenyewe na usisumbue watu badala yake kuwa mstaarabu wa viwango vya juu na dunia itakusaidia kupata kile unachotaka, wakati hufanikiwi kwa sababu ya kukosa ustaarabu wa hali ya juu.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha  ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Join the Conversation

1 Comment

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: