Design a site like this with WordPress.com
Get started

Njia Yenye Ushawishi Kwenye Kila Eneo La Maisha

Siyo njia nyingine bali ni nkia ya kuuliza maswali. Njia ya kuuliza maswali ina ushawishi kwenye biashara, kazi, huduma nk.

Ukitaka kuwashawishi watu na kukubaliana na wewe, tumia njia ya maswali na siyo maelezo.

Mara nyingi binadamu hapendi kuamuliwa, bali anapenda kuamua kupitia kuuliza maswali, yanamjengea fikra sahihi na kufanya maamuzi sahihi.

Ukiwa katika mauzo na mteja, njia ya maswali inamfanya mtu ashawishike kununua na siyo kuuziwa. Watu hawapendi kuuziwa ,ila wanapenda kununua na kupitia njia ya maswali mtu ndiyo anaweza kununua kwani utamuuliza anataka nini na kisha kuja na jibu sahihi kwa kile anachotaka.

Kwa mfano, mwanafalsafa Socrates enzi za uhai wake, alikuchukuliwa ndiyo mtu mwenye hekima kuliko wote. Unajua kwa sababu gani?
Kwa sababu ya kuuliza maswali.

Alichokuwa anakifanya Socrates ni kuuliza maswali mpaka mtu aweke fikra zake kwa usahihi.

Nguvu ya maswali ipo kwenye kumfanya mtu aone amechagua kufanya kitu bila kulazimishwa. Kwa mfano, kwa mteja, unapaswa kumuuliza anataka nini ndiyo umuuzie lakini kumuuzia kitu ambacho mteja hataki hapo unakuwa unazingua kwa sababu wateja hawapendi kulazimishwa kuuziwa bali wanapenda kununua.

Katika kuuliza maswali, kuna mfanya mtu ajielezee zaidi mwenyewe na hivyo kuelewa zaidi kuliko kukazana kumwelezea.

Katika maisha yako, usiwe mtu wa maelezo zaidi, kuwa mtu wa maswali zaidi na utajifunza mengi kupitia wengine kupitia kuuliza maswali.

Maswali yanatusaidia kujua mengi kupitia wengine, hivyo ukitaka kufanikiwa kwenye maisha usiwe mtu wa maelezo bali kuwa mtu wa kuuliza maswali na utajenga ushawishi haraka sana.

Hatua ya kuchukua leo; tumia njia ya kuuliza maswali ina ushawishi kwenye kila eneo la maisha yako.

Kuuliza maswali iwe njia yako kuu ya kuwashawishi watu kukubaliana na wewe. Kumbuka, kuuliza maswali kuna ushawishi mkubwa kuliko kuwapa watu maelezo mengi.

Ukitaka kujua mengi juu ya mtu, ni kupitia maswali, ukawe mtu wa kuuliza na utajifunza mengi sana.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha  ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: