Design a site like this with WordPress.com
Get started

Unafikiri Ni Nini Kinakuzuia Usifanikiwe?

Watu wengi wamekuwa wanafikiri kwamba kinachowazuia kufanikiwa ni vile walivyo.

Lakini, ukweli ni kwamba, kinachokuzuia wewe usifanikiwe ni kile ambacho unajaribu kukikimbia.
Kile ambacho unafikiria siyo ndicho kinachochukua muda na nguvu zako nyingi na kukuzuia kufanikiwa.

Unachotakiwa kufanya ni, kujijua wewe ni nani, na unataka nini, kisha ukafanya maamuzi sahihi ya kuendesha maisha yako kwa kufanyia kazi kile unachotaka.

Ikiwa basi utafanya hivyo, nakuhakikishia utapunguza sana ugumu wa safari yako ya mafanikio.

Pata picha unavyopoteza muda na nguvu nyingi kwenye mambo ambayo hayaendani na wewe, pale unapojilinganisha na wengine.

Unapojaribu kuwaiga wengine au kufanya kwa sababu tu wengine wanafanya hata kama hayana maana kwako.

Utajisikiaje rafiki yangu, kama ukichagua kuwa wewe?

Na habari njema ni kwamba, ukichagua kuwa wewe na kufanya yale ambayo ni muhimu kwako utaweza kupiga hatua kubwa sana kwenye maisha yako.

Hatua ya kuchukua leo; usijifikirie siyo kwani ndiyo kitu kinachokupa muda na nguvu zako nyingi.
Unachotakiwa kufanya, ni kuamua unataka nini na kisha kuwa yule unayemtaka kuwa.

Usipoteze muda kuhangaika na kila kitu, vitakuja kukupoteza. Jifunze tu kutoka kwa taasisi ya benki, wanayo hela na wataalamu na wabobezi wa masuala ya fedha lakini ulishawahi kusikia benki wanahangaika na kila aina ya fursa inayojitokeza?
Kwa nini wasizichangamkie na hela za mtaji wanazo?
Jua kazi yako na fanya kazi yako achana na kuhangaika na mengine.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha  ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: