Design a site like this with WordPress.com
Get started

Sanaa Iliyosaulika Lakini Yenye Nguvu Kubwa

Kusikiliza kwa makini ni Sanaa Iliyosaulika lakini yenye nguvu kubwa sana ya ushawishi.

Ndiyo maana una mdomo mmoja na masikio mawili, kwamba unapaswa kusikiliza zaidi kuliko kuongea.

Watu wengi huwa ni waongeaji sana na kitu kinachowazuia wasiweze kuwajua wengine na kuwashawishi.

Kwenye kitabu cha How I Raised Myself From Failure to Success in Selling, mwandishi Bettger anatushirikisha haya, anatuambia shirika kubwa liliwahi kuandika ujumbe huu wa watu wake wa mauzo; “Unapoangalia maigizo, angalia jinsi waigizaji wanavyosikiliza kwa makini. Ili uwe mwigizaji mzuri,, lazima uwe msikilizaji mzuri pia. Pale unapokuwa msikilizaji mzuri, yule anayeongea anavutiwa kuendelea kujieleza zaidi kitu kinachokupa nafasi ya kuwajua kwa undani.

Hilo linakupa nguvu kubwa ya ushawishi, kwani hata kabla hujamwambia mtu kitu, kwa jinsi ulivyomsikiliza, anakuwa tayari ameshawishika na wewe.

Hatua ya kuchukua leo; kuwa kinyume na wengi na kuchagua kuwa msikilizaji badala ya mwongeaji kwani utaweza kuwa na ushawishi mkubwa kwa watu.

Watu wengi wana maumivu ya ndani lakini hawajapata watu wa kuwasikiliza na kutoa yale yanayowasibu, tiba ya watu wengine ni kusikilizwa tu na wanakuwa wanapona.

Kusikiliza kwa makini ni sanaa ambayo ina nguvu siyo tu kwenye mauzo, bali kwenye mahusiano yote ya watu. Nenda leo kawe msikilizaji makini na unayejali, thamini kile anachoongea mtu kwa kumpa umakini.
Sikiliza lakini sikiliza kwa umakini na kupunguza kuongea sana, wape watu wengine nafasi ya kuongea na wewe sikiliza zaidi.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha  ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: