Design a site like this with WordPress.com
Get started

Tahadhari; Usikosee Wito Wako

Kukosea wito wako, ni sawa na mtu anayefanya kazi sana halafu haoni matokeo anayozalisha.

Na hakuna kitu kigumu kama kujua wito wako, ukikosea wito ni kama vile umepotea njia.

Kitu muhimu ambacho ningependa uondoke nacho hapa leo ni kwamba utafanikiwa zaidi iwapo utafanya kazi au biashara inayoendana na wito uliopo ndani yako.

Achana na kufanya mambo ambayo yako nje yako, hutapata matokeo mazuri unayotaka kuyaona kwenye maisha yako.

Fanya kile unachopenda au kile ambacho una kipaji nacho. Utafanya vizuri zaidi kuliko kukazana na kufanya kile ambacho hakiendani na wewe.

Wito wako uko pale kwenye kile unachopenda kufanya. Na ukifanya kile unachopenda kufanya hakika hata utakatifu wako utaupata hapo.

Kupitia kile unachopenda kufanya ndipo mahali ambapo nyota yako ya mafanikio makubwa ilipo.

Usifanye kitu ilimradi umefanya kwa sababu kinachomfanya mtu afanikiwe siyo kile anachofanya bali namna anavyokifanya.

Ndiyo maana nasema, ukipatia wito, yaani ukifanya kile unachopenda kufanya kwa moyo wako wote lazima utapata mafanikio makubwa.

Hatua ya kuchukua leo; Fanya kile unachopenda kufanya na utaona mafanikio makubwa.

Kufanya kile usichopenda kufanya unakuwa kama mtu aliyekosea wito. Unapofanya kile unachopenda kufanya unakuwa umepatia wito na unajisikia vizuri pale unapofanya.

Wito ni kufanya kile unachopenda kufanya na unakuwa tayari kufanya bila hata malipo. Kwa chochote unachofanya fanya kwa moyo na mafanikio makubwa yatakuja yenyewe.

Maajabu na nguvu za kutenda miujiza ya mtu yako kwenye kufanya kile anachopenda kufanya nje na hapo ni kuhangaika tu.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha  ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: