Design a site like this with WordPress.com
Get started

Kama Unataka Kuuza Chochote Kile, Tafuta Kundi Hili

Kama unavyojua, maisha ni mauzo, lazima uuze kitu fulani ili upate fedha. Bila kuuza, ni wazi hakuna kipato utakachoingiza.

Ili uweze kuuza chochote kile, unapaswa kutafuta kundi lenye njaa kali, kisha unawauzia kundi hilo chakula au kile wanachotaka ili kushibisha njaa yao.

Nadhani unapata picha, mtu akiwa na njaa hasa, atanunua chakula kwa namna yoyote ile.

Sasa tukija katika dhana ya mauzo na masoko watu huwa wanakosea kitu kimoja..

Watu wengi huwa wanakosea kwa kuanza na bidhaa kisha wanakuja kutafuta soko. Hili ni kosa kubwa sana katika masoko na mauzo.

Ili uweze kufanikiwa kwenye mauzo, anza na kutafuta soko kwanza, kisha tafuta bidhaa. Kwa mfano, kabla hujalima matikiti, tafuta kwanza soko la matikiti, kisha lima. Cha kushangaza watu wanaanza kulima matikiti halafu baadaye wanakuwa hawana soko la kuuzia matikiti waliyolima. Ndiyo maana watu huwa wanalalamika kwamba, kilimo au kitu fulani kimewapiga yote hayo ni kwa sababu ya kuanza na bidhaa badala ya kuanza na soko.

Tafuta njaa ya watu iko wapi, jua watu wanataka nini kwanza kisha wape suluhisho kwenye kile wanachokitaka.

Ukianza na bidhaa utatumia nguvu kubwa sana kupata soko. Utakuja kuchukia hata kile unachofanya utajihisi huna bahati na una kisirani au mikosi kumbe tu, ulishindwa kusoma soko linataka nini wewe ulikuja na bidhaa zako unazojua mwenyewe.

Hatua ya kuchukua leo; kwa biashara yoyote unayofanya au unayotaka kufanya anzia sokoni.

Yaani anza kwa kuangalia uhitaji ambao tayari watu wanao, kisha njoo na suluhisho.

Kwa kufanya hivyo, kazi itakua rahisi kwako kuliko ukianza na suluhisho halafu uanze tena kutafuta wale wanaohitaji hilo suluhisho. Jua njaa ya watu iko wapi na Kisha wape chakula wanachotaka.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha  ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: