Design a site like this with WordPress.com
Get started

Usiwe Kopo Linaloelea Juu Ya Maji Likiwa Limefungwa

Ukichukua kopo la maji au chupa ya maji halafu ukaifunga na kuitupia kwenye mto, bahari, au ukaiweka bombani ikiwa imefungwa kamwe maji hayawezi kuingia ndani.

Hii ina maana gani katika maisha yetu ya kawaida?

Watu wengi huenda wanafanya kile wanachopaswa kufanya lakini hawapati matokeo mazuri yanayofanana na juhudi wanazoweka. Yaani wako kwenye maji lakini hawayafaidi yale maji.

Kwa sababu moja tu hawajafungua vifuniko vya chupa yao ili maji ya ingie.

Huenda wako watu wengi tu, hawajafungua vifuniko vya chupa zao ndiyo maana maji hayaingii ndani.

Unaweza ukawa mtu unayehudhuria ibada zote, uko kwenye kila kikundi cha dini lakini hupati zile neema zinazotokana na mahali husika. Shida ni kwamba, watu wako kiimani kwa nje lakini kwa ndani hawajafungua mioyo yao ili zile neema ziweze kuingia.

Ni kama vile chupa ambayo iko kwenye maji, lakini haiingizi maji ndani kwa sababu imefungwa.

Kwenye haya maisha unaweza ukahangaika na vitu vingi sana lakini usipate kitu kwa sababu moja tu hujafungua kifuniko cha kopo kuruhusu maji yaingie ndani.

Mfano mwingine, mtu anafanya kazi kweli na anapata fedha lakini maisha yake ni ya shida mno. Anaishi bila akiba, madeni ni mengi, matumizi yasiyokuwa na ulazima ni mengi. Changamoto ya mtu kama huyu ni kwamba hana elimu ya fedha, angeweza kujifunza elimu ya fedha na kujua jinsi fedha zinavyofanya kazi angeweza kufungua kifuniko cha kopo na kuruhusu maji kuingia ndani.

Unaweza ukawa unanunua vitabu, unasoma lakini maisha yako hayabadiliki kwa nini? Kwa sababu huyaishi yale unayopata kwa vitendo. Unakuwa huna tofauti na kopo linaloelea juu ya maji lakini maji hayawezi kuingia ndani mpaka ufungue kifuniko au kizibo.

Hatua ya kuchukua leo; jitafakari ni eneo gani la maisha yako hujaruhusu kile unachotaka kuingia ndani?

Kama unataka maji yaingie ndani ya chupa yako, tafadhali fungua kifuniko ili maji yaweze kuingia ndani. Usilalamike huna maji wakati uko kwenye maji kumbe shida yako hujafungua kifuniko kuruhusu maji yaingie.

Ukiona mambo yako hayaendi sawa, jua kuna mahali unakosea, jua kuna mahali umefunga chupa na maji yanashindwa kuingia ndani.

Rafiki, chupa inayoelea juu ya maji huku ikiwa imefungwa kamwe maji hayawezi kuingia ndani.
Huenda ukawa unajua kila kitu, yaani uko kwenye maji, lakini kama hufanyii kazi yale unayojua kamwe huwezi kuona mafanikio makubwa kwenye maisha yako. Yaani hapo hujafungua kifuniko kuruhusu maji yaingie ndani ya chupa.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha  ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: