Design a site like this with WordPress.com
Get started

Sheria Namba Moja Ya Kushinda Na Kushikilia Kuaminika Na Wengine

Kwa dunia ya sasa hivi, uaminifu umekuwa ni bidhaa adimu, kamwe usitegemee kuipata kwa kila mtu. Uaminifu wa kitu chochote kile huwa unaanza na sisi wenyewe kwa mfano, Kama unapanga wewe mwenyewe halafu hufanyi hapo unakuwa siyo mwaminifu kwako mwenyewe.

Ili uweze kuaminika lazima uwe na sifa za kuaminika. Mtu yeyote aliyejijengea sifa za kuaminika ni rahisi kukubaliana na watu na kujenga ushawishi mkubwa sana.

Ili kuweza kushinda na kushikilia kuaminika na wengine sheria namba moja unayopaswa kuitumia ni kuwa mwaminifu mara zote.

Falsafa moja ya watu wa Charted Life Underwriter inasema hivi; katika mahusiano yangu yote na mteja nitakuwa nafuata sheria hii ya ufanyaji kazi; mara zote nitampa mteja huduma ambayo mimi mwenyewe ningejipa kama ningekuwa ndiyo mteja huyo.

Kama wewe ni muuzaji wa huduma yoyote ile unayotoa iwe umejiajiri au umeajiriwa mara zote toa huduma ambayo wewe mwenyewe ungependelea kupewa.

Kama ni mteja, mhudumie kama vile wewe mwenyewe ungependa ujihudumie.

Hatua ya kuchukua leo; Kwa chochote kile unachofanya, mara zote kuwa mwaminifu.

Ili uweze kushinda na kushikilia kuaminika na wengine mara zote kuwa mwaminifu. Haijalishi uko peke yako na na watu wengi, kuwa mwaminifu na hii ni moja ya sifa inayolipa sana duniani.

Ukiwa mwaminifu na ukaaminika tayari ni mtaji namba moja ambao unaweza kukusaidia kufanya makubwa sana kwenye maisha yako.

Kitu kikubwa cha kuondoka nacho hapa ni kuwa mwaminifu mara zote.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha  ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: