Design a site like this with WordPress.com
Get started

Usipofanya Kazi Yako Asili Itakuadhibu

Ukichunguza sababu halisi za watu kuwa hivyo walivyo leo wasababishi wakubwa ni wao wenyewe.

Inawezekana ni uvivu, uzembe au ujinga ndiyo unamfanya mtu kubaki katika mkwamo au kuendelea kupata matokeo yale yale.

Ujinga ni kufanya kitu kile kile kwa mtindo ule ule halafu unategemea kupata matokeo tofauti.

Kama hufanyi kazi yako vizuri, kwenye eneo lolote lile la maisha yako, asili Itakuadhibu.

Kama wewe ni mwanandoa halafu unaishi kinyume na falsafa ya ndoa jua asili Itakuadhibu.

Kama wewe ni mfanyabiashara na hufanyi vile vitu ambavyo biashara inataka ufanye jua asili itakuadhibu.

Asili huwa haina huruma na mtu, itakuadhibu vibaya endapo utashindwa kufanya kazi yako.

Haijalishi unafanya kwa kujua au kwa kutokujua asili huwa haingalii hilo yenyewe inakupa kile unachostahili.

Na kwenye maisha unapokea sana kile unachotoa. Usitegemee miujiza yoyote kuweza kutokea wakati huna mchakato wowote unaofanya.

Kama mzazi umepewa jukumu la kulinda watoto wako na ikitokea hutimizi wajibu wako asili itakuadhibu.

Huwezi kuimbia asili, huwa inaona kile unachofanya na habari njema ni kwamba asili huwa haina upendeleo na mtu.

Asili inalinda kila jasho la mtu analoweka sehemu fulani, hivyo basi, unapofanya kazi yoyote jua kabisa hakuna juhudi yoyote ile inayokwenda bure.

Huenda ikawa ni rahisi kukwepa majukumu yako lakini kumbuka kwamba huwezi kukwepa matokeo yake.

Hatua ya kuchukua leo; ili asili isikuadhibu tafadhali fanya kile unachopaswa kufanya kwa uaminifu mkubwa sana.

Usifanye chochote kile kwa namna isiyofaa jua kabisa unapofanya kazi nzuri utapata matokeo mazuri na unapofanya kazi ya hovyo utapata matokeo ya hovyo.

Jitahidi sana kujipenda wewe mwenyewe kwa kufanya kile kilicho bora. Penda wengine na penda sana kile unachofanya.

Pale unapoona mambo hayaendi jiulize ni wapi umeikosea asili? Kwenda kinyume na asili ndiyo chanzo cha kupata matokeo tofauti na matarajio yetu.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha  ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: