Design a site like this with WordPress.com
Get started

Usimpe Mtu Ahadi Ya Kuendelea Kutegemea Wakati Huna Uhakika Wa Kumpatia

Kwenye jamii zetu watu wamekuwa ni mabingwa wa kutoa ahadi na inafikia mahali ahadi zinawafunga watu na hata kukosa raha kwa sababu kila akiangalia amezungukwa na ahadi nyingi alizoamua kuahidi kwa hisia.

Maisha ni yako na una uamuzi wa kutoa pale unapojisikia kutoa na siyo lazima. Usijifunge na ahadi, kama kitu huna uwezo nacho kutoa sema sitoweza kuliko kuahidi na kumpa mhusika mategemeo hewa.

Kwa mfano, tumekuwa na michango ya harusi kila mara ya kuweza kuwawezesha wengine katika tafrija zao. Watu wengi wamekuwa wanakamatwa na ahadi wanazotoa, mtu amekuwa na kadi nyingi za harusi mpaka zinamwelemea badala ya kukataa na kusema ukweli pale anapopewa anaendelea kutoa ahadi kwa wahusika na huku baadaye akiendelea kulalamika.

Uwe huru na maisha yako, pangilia kabisa kwa mwaka utachangia watu wangapi, na idadi ya watu hao ikishafika mwambie mtu kuwa huwa  unapangilia idadi ya watu wa kuwachangia, lakini kwa sasa idadi hiyo imeshajaa na sina tena bajeti ya kuchangia.

Au mwambie mtu ukweli kuliko kumpa matumaini kwamba utamchangia wakati unajua kabisa hutoweza kumchangia.

Kutokutoa kwako mchango sehemu yoyote hakutoweza kukwamisha zoezi lisiendelee kwa sababu wewe siyo kiranja wa dunia kwamba bila wewe mambo hayawezi kwenda. Utoe au usitoe kile kilichopangwa kitaendelea bila hata ya wewe kutokutoa.

Usiishi kiwasiwasi kwamba usimpomchangia mtu na wewe hutakuja kuchangiwa. Usiingie kwenye huu utumwa, kuwa huru na maisha yako.

Unapotaka kufanya jambo lako jiandae wewe mwenyewe kwanza na siyo kusumbua watu wengine. Watu wanazo changamoto zao binafsi zinazowakabili hivyo siyo vema kuwaongezea tena changamoto nyingine.

Kama kitu huwezi kukifanikisha mwenyewe jipange, usiwasumbue watu au fanya kile kinachowezekana ila usiamue jambo kuwategemea watu wengine watakusaidia kulikamilisha.

Kuishi maisha ya kutegemea ahadi za watu wengine ndiyo zilete mapinduzi makubwa kwenye maisha yako huko ni kujidanganya wewe mwenyewe.

Hatua ya kuchukua leo; usiahidi ukiwa na hisia yoyote ile.
Usiwape watu matumaini hewa ambayo unajua kabisa hutoweza kuyakamilisha.

Sina uhakika kama itakufaa lakini kwenye maisha yako jifunze kusema hapana na utajiepusha na matatizo mengi sana. Ndiyo unazosema kila wakati ndiyo zinakuumiza kwa kukuingiza kwenye matatizo yasiyokuwa na ulazima kwako.

Fanya kile ambacho kipo ndani ya uwezo wako na kile ambacho kipo nje ya uwezo wako achana nacho, waachie mwenye mamlaka wakabiliane nalo.

Usifanye jambo ili kuwaridhisha watu na wewe kuonekana umefanya hilo ni kosa kisaikolojia na litakuja kukugharimu baadaye.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha  ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: