Design a site like this with WordPress.com
Get started

Hakuna Mfanyabiashara Anayeweza Kufanikiwa Kwenye Biashara Yake Bila Kujua Kitu Hiki Hapa

Hakuna mtu anayeweza kufanikiwa kama haijui vizuri biashara yake kwa undani.

Na changamoto ya watu wengi ya kutozijua biashara zao ni kwa sababu ya kushindwa kujifunza kwa vitendo na uzoefu.

Hata kama umewaajiri watu wakusaidie kwenye kile unachofanya, hakikisha unakijua wewe mwenyewe vizuri sana na kwa undani.

Unakuta hata waajiri wengi wanadanganywa na wafanyakazi wao kwa sababu hawajui biashara zao vizuri.

Ili ujue biashara vizuri, kuwa na wewe mfanyaji.

Kuwa mtu anayejua kusaka wateja, kukamilisha mauzo na kuhudumia wateja.

Utawafundishaje wengine kama wewe hujawa bora? Kuwa bora kwanza wewe mwenyewe kwa kukijua vizuri kile unachofanya kiasi kwamba hakuna atakayeweza kukupuuza kwenye biashara yako.

Kama huijui biashara yako, asili Itakuadhibu kwa kupata hasara kila siku.

Hatua ya kuchukua leo; hakikisha unakijua kwa undani kile unachofanya biashara yako.

Lazima ujue kila kinachohusika kwenye biashara yako na usitegemee mtu mwingine afanye kwa ajili yako.

Biashara ni yako, tegemea juhudi zako binafsi ili iwe bora, hakuna anayeweza kujali kama wewe unavyojali wewe ndiyo unajua namna gani umepata fedha zako kwa shida kuanzisha biashara uliyokuwa nayo.

Chochote kile ambacho unafanya na umewekeza fedha zako, hakikisha macho yako yote yanakuwa pale.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha  ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: