Design a site like this with WordPress.com
Get started

Chochea Moto Huu Ili Uendelee Kuwaka

Unapaswa kuchochea moto wa hamasa uliopo ndani yako. Hamasa ni kama moto, usipouchochea huwa unazima.

Ili moto uendelee kuwaka ,lazima uchochewe, kuwepo na nishati na hewa ya oksijeni.

Vile vile kwenye hamasa, unaweza kuhamasika mara moja, lakini kadiri muda unavyokwenda hamasa hiyo inapungua.

Unapaswa kuchochea hamasa yakko kila siku.

Unapaswa kujikumbusha kule unakoenda na jinsi maisha yako yatakuwa bora ukifika.

Lakini pia, unapaswa kuwaangalia wale ambao wameweza kupiga hatua kubwa na kuhamasika kwamba inawezekana.

Kila hatua ndogo unayopiga na ukakamilisha, itumie hiyo kama hamasa kwako kupiga hatua zaidi na kufanya makubwa.

Kwa nini kubwa ambayo unayo ndani yako, ikuchochee kufanya makubwa zaidi na kuhamasika zaidi.

Hatua ya kuchukua leo; kila ushindi mdogo unaoupata utumie kupata ushindi mkubwa zaidi.

Kwahiyo, endelea kuchochea moto wa hamasa ndani yako. Usikubali moto uzime, kila siku jikumbushe ndoto kubwa ulizonazo, maono makubwa uliyonayo na kwa nini kubwa inayokusukuma wewe kufanya kile unachopaswa kufanya. Kwa njia hii, utakua unaiwasha moto hamasa yako kila mara.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha  ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: