Hii Ndiyo Njia Rahisi Ya Kupokelewa Kokote Unakokwenda

Kama unataka kupokelewa kokote unakokwenda, kila mtu unayekutana naye mpe tabasamu, tabasamu la kweli kabisa kutoka ndani yako. Kuwa na sura ya kisirani inasababisha kujikosesha bahati kwenye kila eneo la maisha yako. Kama una fanya biashara na huna tabasamu funga hiyo biashara yako kwa sababu tabasamu ndiyo linawavuta watu kuja kwako. Ukiona huuzi jaribu kujichunguza …

Sababu Kubwa Kwa Nini Wauzaji Wanashindwa Kuuza

Kutoka kwenye kitabu cha How I Raised Myself From Failure to Success in Selling, mwandishi Frank Bettger anatushirikisha kwamba sababu kubwa inayopelekea wauzaji wengi kushindwa kuuza ni kuongea sana. Tabia ya kuongea kupitiliza ni chanzo cha wengi kushindwa kuwashawishi wengine kukubaliana nao. Na ubaya wa tabia ya kuongea sana hakuna mtu atakayekuambia kwamba unaongea sana. …

Dunia Huwa Inampisha Mtu Huyu

Dunia inampisha yule ambaye anajua wapi anapokwenda. Kama hujui wapi unapokwenda dunia haiwezi kukupa njia. Ni kawaida katika maisha, pale mtu anapopanga kufanikiwa na kupiga hatua zaidi kwenye yake, ndipo vikwazo vya kila aina vinaibuka. Hii ni njia ya dunia kukupima kama kweli umejitoa kufanikiwa zaidi. Na yule ambaye anaonesha nia, dunia huwa inampisha yule …

Kosa Wanalofanya Wale Wanaoingia Kwenye Biashara Wanazopenda

Ni muhimu  mtu  kuingia  kwenye  biashara  inayohusisha  kitu  anachopenda  au  ambacho ana  uzoefu  nacho.  Lakini lipo  kosa  moja  ambalo  wengi wanafanya  na  linawagharimu. Kosa  hili  ni kujua  zaidi kile  ambacho  wanafanya  kuliko  kujua  biashara  yenyewe. Kwa  mfano  kama  mtu  anajua  na  anapenda  kupika  mikate,  basi  anaanzisha  biashara  ya mikate,  na  kuendelea  kujifunza  kuhusu  mikate. Hapa  …

Usitake Kila Mtu Ajue Kitu Hiki Kuhusu Wewe

Si vema kila mtu ajue maisha yako binafsi ila wale ambao ni watu muhimu kwako. Usiruhusu kila mtu ajue maisha yako binafsi, kwa sababu kwa kufanya hivyo unawapa watu nafasi ya kutumia taarifa hizo kukuangamiza. Mitando ya kijamii siku hizi imekuwa ni sehemu ambayo watu wamekuwa wanaanika mambo yao binafsi. Hii inapelekea watu kukusanya taarifa …

Vitu Viwili Vinavyoweza Kukuhamasisha Kuendelea Kufanya Kila Siku

Hamasa huwa haidumu, ni kama moto wa kuni, ili uendelee kuwaka unatakiwa kuchochewa. Vipo vitu viwili ambavyo vinaweza kukupa kichocheo cha kuendelea kufanya kila siku. Cha kwanza, ni thamani unayotoa, pale unapoona thamani unayotoa na namna inavyowasaidia wengine, unapata hamasa ya kufanya zaidi. Cha pili ni kusudi. Yaani unapojua kusudi la maisha yako na kulifanyia …

Ukitaka Mafanikio, Penda Kitu Hiki

Kwenye maisha tunapata kile ambacho tunakivumilia na si viginevyo. Ukitaka kufanikiwa kwenye maisha yako, basi upende mchakato wote. Yule anayevumilia kukaa kwenye mchakato mpaka mwisho ndiyo anafanikiwa kupata kile anachotaka kwenye maisha yake. Ni wangapi wameanza na wameishia njiani? Hata mtu hajapata kile anachotaka anashindwa kuvumilia kukaa kwenye mchakato na anaishia njiani. Mafanikio  hayatatokea  mara  …

Njia Wanayotumia Wateja Wengi Kukutoroka

Kwa kuwa wewe ni muuzaji bora kuwahi kutokea, unapaswa kuwa vizuri sana kwenye eneo la mauzo kwani mauzo ndiyo yanaleta fedha mifukoni. Hakuna watu wajanja kama wateja, wanazo mbinu nyingi wanazotumia pale wanapokuwa hawataki kununua kwako. Na siyo kwamba hawana hela, hela wanazo na wakiamua kukupiga chenga wanakujibu jibu ambalo halitakufanya uumie. Wateja wanajua sisi …

Tatizo Lako Linatatuliwa Na Fedha?

Ukijaribu kuchunguza changamoto nyingi ambazo watu wanakabiliana nazo zinatokana na kukosa fedha za kutatua changamoto zinazowakabili. Kama una changamoto na ukipata fedha unaweza kuitatua basi wewe hapo changamoto yako ni kwamba huna fedha ya kutatua changamoto zinazokukabili. Kama fedha inaweza kutatua changamoto uliyonayo, basi pambana uweze kupata fedha zaidi. Mwandishi na mfanyabiashara Kevin O'Leary anasema …

Nilichojifunza Kwenye Haya Maisha

Pale tunapokutana na changamoto au mambo hajaenda kama vile tunavyotaka sisi huwa kitu cha kwanza tunachofikiria ni nani amesababisha lakini huwa tunajisahau na sisi tumehusikaje kutokea kwa kile kilichotokea. Hata sisi wenyewe huwa tunachangia sana kwa changamoto mbalimbali katika maisha yetu lakini huwa hatukubali tunajiona sisi ni watakatifu. Kwenye kila kitu kinachotokea kaa chini jiulize …

Design a site like this with WordPress.com
Get started