Design a site like this with WordPress.com
Get started

Njia Wanayotumia Wateja Wengi Kukutoroka

Kwa kuwa wewe ni muuzaji bora kuwahi kutokea, unapaswa kuwa vizuri sana kwenye eneo la mauzo kwani mauzo ndiyo yanaleta fedha mifukoni.

Hakuna watu wajanja kama wateja, wanazo mbinu nyingi wanazotumia pale wanapokuwa hawataki kununua kwako.

Na siyo kwamba hawana hela, hela wanazo na wakiamua kukupiga chenga wanakujibu jibu ambalo halitakufanya uumie.

Wateja wanajua sisi wote ni viumbe vya hisia hivyo hawezi kukuambia mubashara yaani live kwamba hataki kitu fulani. Bali atakuambia nitakutafuta nikiwa tayari.

Siyo tu kwenye mauzo bali hata kwenye maisha yetu ya kawaida, ili mtu asikuambie hapana, anakutafutia jibu ambalo hutaumia lakini ukipewa hilo jibu biashara yake na yako ndiyo inakuwa imefikia kikomo hapo.

Mteja akikuambia nitakutafuta nikiwa tayari, usikubaliane naye kirahisi. Muulize, lini utakua tayari? Wengi wanakuwa hawana majibu, wanakujibu hivyo ili wakuridhishe tu. Ukishakuwa mtu wa kuhoji na kushawishi atakuwa tayari kununua.

Au muulize nini kinachokufanya usiwe tayari kununua? Wengi utaona hawana sababu, hivyo wakishakuwa hawana sababu za mashiko huwa wanajikuta wananunua tu wenyewe.

Hatua ya kuchukua leo; unapokuwa kwenye mauzo ya kitu chochote kile, mtu akikuambia nitakutafuta nikiwa tayari usikubaliane naye kabisa, mwambie lini utakua tayari au kipi kikubwa ambacho kinakuzuia usiwe tayari leo?

Kwa hiyo, Ng’ang’ania hapo kwenye maswali mpaka akupe jibu ambalo ni la kweli. Na akikuambia siku fulani kwa kukupa ahadi, endelea kumfuatilia kwenye ahadi hiyo. Watu huwa wakiahidi na wasipotekeleza huwa wanajisikia vibaya hivyo kuwa mfuatiliaji wa karibu siyo tu kwenye mauzo bali hata kwenye maisha ya kawaida.

Kama muuzaji, kuwa makini wateja wengi wanakupiga chenga kwa kukuambia watakutafuta wakiwa tayari.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha  ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: