Design a site like this with WordPress.com
Get started

Nilichojifunza Kwenye Haya Maisha

Pale tunapokutana na changamoto au mambo hajaenda kama vile tunavyotaka sisi huwa kitu cha kwanza tunachofikiria ni nani amesababisha lakini huwa tunajisahau na sisi tumehusikaje kutokea kwa kile kilichotokea.

Hata sisi wenyewe huwa tunachangia sana kwa changamoto mbalimbali katika maisha yetu lakini huwa hatukubali tunajiona sisi ni watakatifu.

Kwenye kila kitu kinachotokea kaa chini jiulize hivi nimehusikaje au nimechangiaje kutokea kwa hichi kilichotokea?

“Nilichojifunza  kwenye  haya  maisha  ni  labda  uchague kujiadhibu  mwenyewe  au  dunia  itakuadhibu.  Nimechagua  kujiadhibu mwenyewe.”.

Rafiki, wewe umechagua kujiadhibu au umeacha tu dunia ikuadhibu?

Ni bora ujiadhibu mwenyewe mapema kuliko kusubiri dunia ije kukuadhibu. Dunia huwa inaadhibu vibaya bila huruma, jitume kabla hujatumikishwa.

Chukua hatua mara moja kwenye eneo lolote la maisha yako unaloona haliko sawa. Usisubiri mpaka kukumbushwa kwa gharama.

Maisha yako ni jukumu lako, chagua kujiadhibu mwenyewe kabla dunia haijakuadhibu.

Usipochagua kujiadhibu mwenyewe, dunia itakuadhibu.
Mimi nimechagua kujiadhibu mwenyewe je wewe?

Usijionee huruma kujiadhibu kwani usipojiadhibu wewe mwenyewe dunia itakuja kukuadhibu.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha  ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: