Design a site like this with WordPress.com
Get started

Dunia Huwa Inampisha Mtu Huyu

Dunia inampisha yule ambaye anajua wapi anapokwenda.

Kama hujui wapi unapokwenda dunia haiwezi kukupa njia.

Ni kawaida katika maisha, pale mtu anapopanga kufanikiwa na kupiga hatua zaidi kwenye yake, ndipo vikwazo vya kila aina vinaibuka.

Hii ni njia ya dunia kukupima kama kweli umejitoa kufanikiwa zaidi. Na yule ambaye anaonesha nia, dunia huwa inampisha yule ambaye anajua wapi anapokwenda.

Dunia huwa inampisha yule ambaye anajua wapi anapokwenda, mtu ambaye hakati tamaa wala kurudishwa nyuma na magumu anayopitia.

Hatua ya kuchukua leo;
Kama unataka dunia isiwe kikwazo kwako kwenye safari ya mafanikio, jua kwa hakika wapi ni unakwenda na usikubali chochote kiwe kikwazo kwako kufika unakotaka kufika.

Kwenye safari ya mafanikio makubwa, usiangalie matokeo unayopata bali zingatia sana kukaa kwenye mchakato sahihi.
Kuwa king’ang’anizi, kuwa mbishi kiasi kwamba dunia inakupa njia ya kupata kile unachotaka.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha  ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: