Ni muhimu mtu kuingia kwenye biashara inayohusisha kitu anachopenda au ambacho ana uzoefu nacho.
Lakini lipo kosa moja ambalo wengi wanafanya na linawagharimu. Kosa hili ni kujua zaidi kile ambacho wanafanya kuliko kujua biashara yenyewe.
Kwa mfano kama mtu anajua na anapenda kupika mikate, basi anaanzisha biashara ya mikate, na kuendelea kujifunza kuhusu mikate.
Hapa anakutana na changamoto nyingi kwa sababu hajui kuhusu biashara, bali anachojua ni kuhusu mikate.
Ili kuondokana na changamoto hii, unapaswa kujifunza upande wa biashara. Hata kama unajua sana kile unachofanya, jifunze kuhusu biashara.
Vitu muhimu kama masoko, mauzo, mzunguko wa fedha, hesabu za fedha na kadhalika.Vitakusaidia kuendesha biashara yenye mafanikio.
Kama unajua kile unachopenda na huna masoko huwezi kuuza na huuzi kwa sababu watu hawajui kile unachouza.
Masoko ni kuwafanya watu wajue kuhusu biashara yako. Na watu wakishajua biashara yako ni rahisi kuja kupata huduma pale wanapokuwa na uhitaji.
Mauzo, mauzo ndiyo kila kitu kwenye biashara. Kama huuzi basi biashara yako haina uhai. Lazima watu waijue biashara yako na kisha ufanye mauzo. Mauzo ndiyo yanaleta fedha kwenye biashara yako.
Hatua ya kuchukua leo; jitahidi sana kujifunza zaidi masoko, mauzo, jua mzunguko wa fedha kwenye biashara yako.
Ipende biashara yako kwa kufanya kile unachopenda lakini usisahau kujifunza kuhusu biashara yako. Jua mtaji unaozunguka, jua hesabu za fedha kwenye biashara yako.
Jua masoko, mauzo nakadhalika.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog