Kutoka kwenye kitabu cha How I Raised Myself From Failure to Success in Selling, mwandishi Frank Bettger anatushirikisha kwamba sababu kubwa inayopelekea wauzaji wengi kushindwa kuuza ni kuongea sana.
Tabia ya kuongea kupitiliza ni chanzo cha wengi kushindwa kuwashawishi wengine kukubaliana nao.
Na ubaya wa tabia ya kuongea sana hakuna mtu atakayekuambia kwamba unaongea sana.
Ila kinachotokea ni watu wanakuwa wanakukwepa kwa kwa sababu ya kuongea kwako kupitiliza.
Kuongea sana siyo njia sahihi ya kumshawishi mteja bali ni kumpoteza mteja.
Nini unachotakiwa kufanya?
Nenda kwenye hoja moja kwa moja usipoteze muda kwenye maelezo yasiyokuwa na tija.
Hatua ya kuchukua leo; usiongee sana, nenda kwenye hoja moja kwa moja, usipoteze muda kwenye maelezo yasiyokuwa na tija.
Kwahiyo, usiwe muongeaji sana kwenye mauzo, jitahidi sana kuongea kwa ufupi yale ambayo ni muhimu tu.
Watu wana mambo mengi, hivyo usiwapotezee muda wao kwenye mambo yasiyokuwa na tija.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog