Design a site like this with WordPress.com
Get started

Usitake Kila Mtu Ajue Kitu Hiki Kuhusu Wewe

Si vema kila mtu ajue maisha yako binafsi ila wale ambao ni watu muhimu kwako.

Usiruhusu kila mtu ajue maisha yako binafsi, kwa sababu kwa kufanya hivyo unawapa watu nafasi ya kutumia taarifa hizo kukuangamiza.

Mitando ya kijamii siku hizi imekuwa ni sehemu ambayo watu wamekuwa wanaanika mambo yao binafsi. Hii inapelekea watu kukusanya taarifa zako na baadaye kuja kuzitumia kukuangamiza.

Hakikisha watu wanaokujua ni wale ambao ni wa muhimu kwako na siyo kila mtu anapaswa kujua kuhusu wewe.

Hatua ya kuchukua leo; usiyaanike maisha yako hadharani, usitake kila mtu ajue kila kitu kuhusu maisha yako.
Taarifa nyingine zinapaswa kuwa kwako na kwa wale unaowajua tu.

Kwa sababu, huwezi kujua ni mtu gani atachukua taarifa zako na kuzitumia vibaya kujifaidisha.

Kitu cha mwisho, usiruhusu kila mtu ajue vitu hivi vitatu kuhusu wewe, afya yako, familia yako na kipato chako. Watu wakishajua vitu hivyo wataanza kuvitumia kupata maslahi yao.
Chagua watu ambao ni chanya mnaoweza kushirikiana mambo yenu muhimu na siyo kila mtu.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha  ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: