Kwenye maisha tunapata kile ambacho tunakivumilia na si viginevyo.
Ukitaka kufanikiwa kwenye maisha yako, basi upende mchakato wote.
Yule anayevumilia kukaa kwenye mchakato mpaka mwisho ndiyo anafanikiwa kupata kile anachotaka kwenye maisha yake.
Ni wangapi wameanza na wameishia njiani? Hata mtu hajapata kile anachotaka anashindwa kuvumilia kukaa kwenye mchakato na anaishia njiani.
Mafanikio hayatatokea mara moja kama ajali bali ni safari ndefu.
Kuna mchakato mrefu ambao utaupitia mpaka ufikie mafanikio. Unahitaji kufanya kazi kwa juhudi na maarifa, kuwa mbunifu na hata kuwa mvumilivu.
Kama utaruka hatua yoyote ya mchakato huu utashindwa kufikia mafanikio.
Furahia kila hatua unayopitia ya kukufikisha kwenye mafanikio. Maana kila kitu ni muhimu sana kwako.
Hatua ya kuchukua leo; Amini mchakato na kaa kwenye mchakato sahihi na mengine yatakuja yenyewe.
Usiangalie matokeo ya siku moja, jenga nidhamu ya kukaa kwenye mchakato sahihi na matokeo mazuri unayotaka kuyaona kwenye maisha yako yatakuja yenyewe.
Kama utauamini mchakato, kama utaupenda mchakato na kama utafanyia kazi mchakato bila ya kukoma, basi hakuna kitakachokuzuia kufanikiwa aliwahi kunukuliwa Ruben Gonzalez
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog