Kwa utamaduni wa kiafrika ambao tunao, ni vigumu sana mtu kufanikiwa kwa sababu watu wengi wanafanya kazi kimazoea. Huwezi kufanikiwa kwenye kitu chochote kile kama hujaondoa utamaduni wa kiafrika ambao tunao. Utamaduni wa kiafrika hauchochei maendeleo bali unadumaza maendeleo. Pata picha kwenye jamii yako wewe unavyokuwa wa tofauti na jamii inavyokusema. Kwa mfano, jamii zetu …
Naomba Uniombee Ili Niache Hiki Hapa
Kiasili binadamu ni wavivu. Watu wengi wamekuwa hawataki kufanya kitu wanachopaswa kufanya kwa sababu ya uvivu uzembe na ujinga halafu wanaomba uwaombee ili wakae kwenye mchango. Mtu anakua anashindwa kutimiza wajibu wake anamsingizia shetani hivyo anaomba umuombee aache hiyo tabia. Yaani mambo binafsi ambayo yanahitaji nidhamu ya kuamua na kufanya mtu anataka aombewe. Tumpunguzie Mungu …
Imani Isizidi Akili
Amini lakini imani yako isizidi akili. Hii ina maana kwamba, licha ya kuwa na imani kubwa kwenye jambo fulani usikubali imani iamue kila kitu na badala yake tumia akili ulliyopewa kufanya maamuzi. Watu wengi wanakuwa wapofu juu ya vitu vingi kwa sababu wanakuwa wanaweka imani zaidi badala ya akili. Ni jambo zuri mtu kuwa na …
Kukubali Kwa Nje Tu
Watu huwa wanafanya kitu kama wamekubali wao wenyewe kutoka ndani ya mioyo yao. Unaweza ukawahamasisha kadiri uwezavyo na ukakubaliana nao kabisa kwamba watafanya lakini wanakuja kufanya kinyume. Ukiona mmekubaliana na mtu kufanya kitu halafu hafanyi jua alikukubalia kwa nje tu ili kukufurahisha kwa nje. Lakini ile ndiyo kutoka ndani yake haiko. Anaona ni bora akuridhishe …
Jinsi Ya Kujua Thamani Ya Utajiri Wako
Katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa ya ubilionea ni muhimu sana ujijue mpaka sasa una utajiri wa kiasi gani. Kuishi bila kujua una utajiri wa kiasi gani unakuwa kama vile mtu uko gizani. Umeshasikia tajiri fulani, utajiri wake ni kiasi gani, na wewe pia unapaswa kujua. Jinsi ya kujua utajiri wako halisi, CHUKUA THAMANI YA …
Ukiona Choo Kwenye Usingizi Usikitumie
Natumaini ilishawahi kukuta wakati uko mdogo, unaota unaona choo na ukikitumia tu unakuta tayari umeshajikojolea. Ukiona choo kwenye usingizi usikitumie, ina maana gani kwetu? Ukiona mambo ni rahisi sana shtuka.Ukiona mambo yanaenda vizuri kwenye biashara shtuka. Huenda unategwa hapo ili uingie kwenye mtego. Kama unafanya kitu na hakikusumbui, shtuka. Kama una ratiba ya siku ambayo …
Mauzo Hayaishii Pale Anaponunua Bali…
Maisha ni mauzo na yeyote anayeweza kuuza vizuri zaidi ndiye anayefanikiwa. Na utaweza kupata chochote unachotaka kwenye maisha yako kama utaweza kuuza zaidi. Tunauza muda wetu, utaalamu wetu, uzoefu wetu, huduma zetu na hata bidhaa mbalimbali. Pia tunauza mawazo yetu, ushawishi wetu na hata ndoto na maono makubwa tuliyonayo. Mauzo huwa hayaishii pale tu mteja …
Tengeneza Fikra Hizi Kwenye Kila Kazi Na Biashara Unayofanya
Kuna watu wanaamini kwamba kuna kazi au biashara zinazolipa kuliko nyingine. Kila kazi au kwenye kila biashara kuna watu wengi tu wanaotengeneza fedha nyingi na wapo ambao hawatengenezi fedha kabisa. Je, unajua kwa nini ?Kwa sababu kinachowatofautisha wale wanaopata fedha na wale wanaokosa siyo kile wanachofanya bali ni namna wanavyofanya kile wanachofanya. Kama hupati matokeo …
Continue reading "Tengeneza Fikra Hizi Kwenye Kila Kazi Na Biashara Unayofanya"
Acha Kufanya Mambo Yasiyokuwa Sahihi
Ili uweze kwenda mbele, lazima kwanza uache kufanya mambo yasiyokuwa sahihi. Ukiwa ni mtu wa kufanya kazi na kufanyia kazi yale mambo sahihi tu lazima utafanikiwa. Hufanikiwi, kwa sababu unafanya mambo yasiyokuwa sahihi mengi. Ukifanya mambo sahihi, lazima utapata majibu sahihi. Mambo sahihi yanafanya kazi kama ukiyafanyia kazi. Ukiamua tu kufanya mambo sahihi lazima utapata …
Usiwe Na Wasiwasi Na Mtu Huyu
Usiwe na wasiwasi na nafsi yako mwenyewe. Kinachowazuia wengi kufanikiwa ni kuwa na wasiwasi juu ya nafsi zao wenyewe. Na ukishakuwa na wasiwasi huwezi kufanikiwa kwenye maisha yako. Kwa sababu adui mkubwa wa imani ni mashaka. Watu wana wasiwasi juu ya nafsi zao wenyewe kwa sababu walijaribu na kushindwa huko nyuma. Hivyo wanahofia kujaribu tena …