Mpendwa rafiki,
Wote tunajua umuhimu wa kazi, ila sharti la kazi iwe halali na siyo vinginevyo. Usijisifie unafanya kazi kumbe kazi yenyewe siyo halali.
Kuna kazi ambayo watu wengi sana hawaifanyi, kazi ambayo kila mmoja wetu akiifanya inamletea mafanikio makubwa kwenye maisha yake.
Kazi unayopaswa kufanya kila siku ili ikuletee mafanikio makubwa siyo kazi nyingine bali ni kazi kufanya maamuzi. Watu wengi hawafanyi maamuzi ndiyo maana hawafanikiwi katika maisha yako.
Kila mmoja wetu anatakiwa kufanya maamuzi kila siku, bila kufanya maamuzi huwezi kufika kokote kule. Kuna watu wanaogopa kufanya maamuzi katika maisha yao kwa sababau ya kuogopa watu watamchukuliaje.
Rafiki, jukumu la maisha yako ni lako mwenyewe, na unapofanya maamuzi jiangalie kwanza wewe na siyo watu wengine.Ukiwa ni mtu wa ndiyo kwenye kila kitu utachelewa kufanya ya kwako.
SOMA; Usiwe Na Huruma Katika Kufanya Maamuzi Haya
Jaribu kujitawala mwenyewe kwa maamuzi yako siyo kutegemea kuamuliwa maisha na watu wengine. ishi vile utakavyo wewe na fanya maamuzi kila siku ya kufikia kwenye mafanikio makubwa.
Kama unaona hali uliyokuwa nayo haikuridhishi amka na fanya maamuzi magumu. Hakuna kitu kitakachokutoa hapo ulipo na kwenda sehemu nyingine bila kufanya maamuzi.
Maamuzi ndiyo yanayokutoa sehemu moja kwenda nyingine. Binadamu asiyefanya maamuzi hawezi kufanikiwa kwa kitu chochote.
Tuna ushahidi mkubwa sana mafanikio uliyonayo ni matokeo ya maamuzi uliyofanya jana. Ili ufanikiwe unatakiwa kufanya maamuzi magumu. Lazima ukubali kupoteza kitu kizuri ili upate kitu bora. Kama unataka kwenda mkoa b lazima ukubali kuucha mkoa a na kwend b huwezi kuving’ang’ania vyote kwa pamoja.
Chagua moja na fanya maamuzi sahihi. Unapofanya maamuzi jiangalie kwanza wewe kwa sababu ndiyo maisha yako. usiwe mtu wa kumsikiliza kila mtu, jisikilize mwenye ndiyo utafanikiwa. Sauti za watu ni nyingi sikiliza sauti yako.
Hatua ya kuchukua leo; fanya maamuzi sasa sahihi ili uweze kufanikiwa kwenye maisha yako. bila maamuzi hakuna mafanikio yoyote yale.
Kwahiyo, chochote unachotaka lazima ufanye maamuzi kwenye maisha yako ndiyo utapata kile unachokitaka.
Muhimu; kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.
Ukawe na siku bora sana rafiki.
Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com // kessydeo@mtaalamu.net
Asante sana.