Design a site like this with WordPress.com
Get started

Hii Ndiyo Njia Rahisi Ya Kupokelewa Kokote Unakokwenda

Kama unataka kupokelewa kokote unakokwenda, kila mtu unayekutana naye mpe tabasamu, tabasamu la kweli kabisa kutoka ndani yako.

Kuwa na sura ya kisirani inasababisha kujikosesha bahati kwenye kila eneo la maisha yako. Kama una fanya biashara na huna tabasamu funga hiyo biashara yako kwa sababu tabasamu ndiyo linawavuta watu kuja kwako.

Ukiona huuzi jaribu kujichunguza huwa unakuwaje kwa wateja wako, watu waliokuzunguka? Watu wanapenda kununua kwa mtu ambaye ana tabasamu la kweli kabisa kutoka ndani.

Kitendo cha wewe kuwa na tabasamu na wateja wanajikuta wana tabasamu. Hii itakusaidia kuongeza ushawishi, ukubalike zaidi na kuaminika zaidi.

Tumia nguvu ya tabasamu siyo tu kwenye mauzo bali hata unapokutana na watu barabarani, waite watu hao kwa majina yao na kuwasalimia ukiwa na tabasamu kubwa usoni mwako.

Unapokuwa na tabasamu la kweli kwenye uso wako unaonekana kuwa mtu wa mwenye bahati zaidi na hata ukienda popote pale watu watakupokea kwa sababu tabasamu lako litawavuta.

Tabasamu linakufanya uwashawishi watu na kuwa tayari kukubaliana na wewe na kukupa kile unachotaka kwenye maisha yako.

Nguvu ya kutabasamu haipo tu kwenye mazungumzo ya ana kwa ana lakini hata kwenye mazungumzo ya simu.

Hatua ya kuchukua leo; kila mtu unayekutana naye mpe tabasamu la kweli kabisa kutoka ndani yako.

Na sehemu nzuri ya kuanzia ni watu wako wa karibu, anza na mwenza, watoto na marafiki zako na utaona jinsi mahusiano yako yatakavyobadilika.

Kitu cha mwisho, usiende kukutana na mteja au mtu yeyote yule au kuongea na mtu kwenye simu ukiwa huna tabasamu kwenye uso wako.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha  ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: