Kutokujua Sheria Siyo Kigezo Cha Kusamehewa Kosa Lako

Ni kauli ya sheria ambayo inatumika karibu kwenye kila eneo la maisha yetu. Usipofanya kitu kwa sababu hujui usifikiri asili itakuacha salama. Lazima itakupa adhabu ya kutokujua kwako, kwa mfano, unavunja sheria kwa sababu ya ujinga wa kutokujua sheria, usifikiri kutokujua kwako kunaweza kukusaidia, hapana. Angalia sheria za asili zinavyofanya kazi. Watu hawajui misingi ya …

Kila Mtu Anakwenda Kujua Jina Langu

Maisha bila hamasa hayawezi kwenda vizuri sana. Kwa sababu sisi ni binadamu tunapaswa kupata hamasa ili tuweze kujisukuma kufanya kile tunachopaswa kufanya bila kukata tamaa. Kwa kuwa mimi ni Muuza Hamasa, Afisa Mhamasishaji Mkuu CIO (Chief Inspiration Officer na kwenda kukuuzia hamasa ambayo itafanya kila mtu ajue jina lako kupitia kile unachofanya. Kwenye maisha kila …

Kuahirisha Siyo Kitu Kibaya Kama Unahairisha Kwa Ajili Ya Kitu Hiki

Kama unahairisha kitu kibaya kwa ajili kitu kizuri hapo kuahirisha siyo kitu kibaya bali ni kitu kizuri. Kama unahairisha kuweka fokasi kwenye vitu vidogo na kuweka fokasi kwenye vitu vikubwa hapo kuahirisha siyo kitu kibaya. Kama unahairisha kufanya anasa na kufanya uwekezaji basi hapo ni kuahirisha katika mtazamo chanya. Kama unahairisha kuzurura kwenye mitandao ya …

Mfahamu Mtu Ambaye Hana Kazi Ya Kufanya

Huwa ninasikitishwa sana na mtu ambaye anasema kwa sasa sina kazi ya kufanya. Kwa binadamu ambaye uko hai unakosaje kazi ya kufa kufanya? Katika kukaa na kutafakari nikapata majibu kwamba, mtu ambaye hana kazi ya kufanya maana yake ni mtu ambaye hana thamani. Mtu mwenye thamani, hawezi kukosa kazi ya kufanya.Mtu ambaye anatoa thamani kubwa …

Jinsi Ya Kuepuka Kujitengenezea Balaa

Vitu vingi katika maisha yetu, huwa tunavitengeneza sisi wenyewe, kwa mfano, tunatengeneza tabia na kisha tabia zinatutengeneza. Hata wakati mwingine, balaa huwa mtu anajitengenezea, utaweza kushangaa sasa inakuwaje mtu anajitengenezea. Kuna msemo mwingine unasema akili isiyoshughulika inakuwa ni karakana ya shetani. Mtu ambaye ameamka asubuhi na akaupangilia muda wa vizuri, hata shetani ni ngumu kumjaribu …

Viungo Viwili Vinavyohitajika Kwenye Biashara

Ni macho na masikio. Macho yako wewe kama una biashara yanatakiwa kuwa kwenye namba. Unapaswa kujua namba muhimu za biashara yako kama vile mtaji unaozunguka kwenye biashara, idadi ya mauzo kwenye biashara, faida unayopata na kuhakikisha biashara yako inatengeneza masoko mapya kila siku. Huwa tunajinyima fedha nyingi kwenye biashara kwa sababu ya biashara kutokujulikana na …

Jinsi Wazazi Wanavyowachokoza Watoto Wao

Watoto wawili katika familia moja walikuwa wanapata kipigo kikali kutoka kwa baba yao. Siku moja baada ya kupata cha mtema kuni, waliandika maneno haya kwenye chumba cha kulala cha baba yao. " Uwe na huruma kwa watoto wako nao watakuwa na huruma kwako, wako Mungu. " Mtume Paulo wa Tarsus anawaasa wazazi, "msiwachokoze watoto wenu, …

Mafanikio Mengi Ya Kifedha Huwa Yanakuja Na Hili Pia

Mwanamziki wa kimarekani Rick Ross kwenye moja ya wimbo wake mmoja anasema fedha nyingi, matatizo mengi, usiniite bosi yaani more money, more problem don't call me the boss. Mafanikio ya kifedha huwa yanakuja na matatizo makubwa ya kifedha pia. Siyo kwamba ukishakuwa na fedha nyingi ndiyo umeshayapatia maisha yako, yaani huhitaji tena kuhangaika hapana, siyo …

Ifanye Siku Ya Mwenzako Kuwa Bora Kupitia Hiki Hapa

Huwezi kuishiwa pale unapotoa thamani kubwa kwa wengine. Kwa mfano, watu wanakula samaki kila siku lakini ulishawahi kusikia samaki wameisha baharini? Ifanye siku ya mwenzako kuwa bora kupitia kile unachofanya.Kile unachofanya kina msaidia mwenzako kuwa bora kwa namna moja au nyingine. Kuna watu wanakutegemea kupitia kile ambacho, hata kama huoni mrejesho wake, lakini jua kuna …

Rudia Tena Kufanya

Karibu kila mtanzania anajua kuimba wimbo wa Taifa bila shida yoyote ile. Na watu wanaweza kuimba wimbo wa Taifa kwa sababu walivyokuwa shuleni walikuwa wanauimba karibu kila siku. Hii imepelekea hata watu wengi kuunasa kichwani na kuuelewa bila shida. Hapa tunajifunza kitu kikubwa sana, ukitaka watu wakielewe kitu, unapaswa kukirudia rudia kitu mara kwa mara …

Design a site like this with WordPress.com
Get started