Watoto wawili katika familia moja walikuwa wanapata kipigo kikali kutoka kwa baba yao.
Siku moja baada ya kupata cha mtema kuni, waliandika maneno haya kwenye chumba cha kulala cha baba yao. ” Uwe na huruma kwa watoto wako nao watakuwa na huruma kwako, wako Mungu. “
Mtume Paulo wa Tarsus anawaasa wazazi, “msiwachokoze watoto wenu, bali waleeni katika adabu na maonyo ya Bwana”
Ukali wa kupindukia kwa mtoto ni kumchokoza mtoto.
Yapo mambo mengi ambayo wazazi wanafanya wanakuwa wanawachokoza watoto. Watoto wa kikazi hiki huwezi kuwalea kama watoto kikazi chako, unapaswa ucheze na wakati, mbinu uliyotumia huko nyuma haiwezi kuwa sawa na kikazi hiki.
Kumtesa mtoto eti kwa sababu wewe uliteseka na ulipitia magumu sana hivyo na yeye anapaswa kusoma kwa kuteseka kama wewe. Huko ni kumchokoza mtoto.
Mambo yamebadilika unapaswa kutambua hilo kama mzazi, tamaduni nazo zimebadilika na nyakati zimebadilika. Kwa mfano, mzazi kumkataza mtoto kuangalia katuni au mambo yanayowahusu watoto kwenye TV kwa sababu wewe huangalii au hupendi TV huko ni kumchokoza mtoto na kumnyima haki.
Siyo kwamba kila kitu ni kibaya kwenye nyakati hizi, chukua yale ambayo ni mazuri mpe mtoto wako na yale ambayo ni mabaya mkataze. Usimlee mtoto kikoloni maana huko ni kumchokoza mtoto.
Matatizo mengi yanayowapata watoto na vijana ni kutokana na familia zilizojengwa kwenye mchanga kudekeza badala ya kujengwa kwenye mwamba wa nidhamu. Weka msingi imara katika familia yako na walee watoto wako vizuri kwa kuwapa malezi bora ambayo yatawasaidia hata siku ambayo wewe hauko duniani.
Mtoto anapofanya vizuri mzazi unapaswa kufanya kazi ya kuwatia moyo watoto au mtoto wako. Kutowapongeza watoto wanapofanya vizuri ni kuwachokoza watoto.
Waswahili wanasema samaki mkunje angali mbichi. Mpe mtoto wako malezi bora na kumfundisha yale yote ya msingi.
Mfundishe misingi muhimu ya dini yako, maana kila dini ina mafunzo mazuri juu ya malezi ya watoto. Hivyo ukitumia falsafa ya dini utakua umemsaidia mtoto kuwa katika maadili mazuri yanayompendeza Mungu na mwanadamu.
Hatua ya kuchukua leo; usifanye mambo yanayopelekea kumchokoza mtoto. Kama kitu siyo sahihi usifanye mbele kwa mtoto wako na kama kitu siyo kweli usiseme kwa mtoto wako kwa wazazi kugombana na kutukanana matusi.
Mzazi usifanye mambo ya aibu mbele ya mtoto kama vile ulevi kwa kufanya hivyo utakua umemchokoza mtoto.
Mwisho, nakuacha na
Mtume Paulo wa Tarsus anawaasa wazazi, “msiwachokoze watoto wenu, bali waleeni katika adabu na maonyo ya Bwana”
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505//0767101504
https://kessydeo.home.blog