Design a site like this with WordPress.com
Get started

Adhabu Zinawasaidia Watoto Kuelewa Uhalisia Wa Dunia

Wazazi wa siku hizi wanawalea watoto utafikiri wamepata mkataba wa kuishi nao milele. Wazazi hawataki kuwafundisha watoto kukosa. Mtoto akitaka kile anachotaka anapewa mara moja. Hii inamfanya mtoto kuja kuteseka baadaye anapokuja kuingia kwenye uhalisia wa mambo. Watoto wanaharibiwa kwa kukosa adhabu kuliko kuharibiwa na adhabu. Kumekuwa na harakati nyingi za kufuta adhabu kwa watoto …

Jinsi Wazazi Wanavyowachokoza Watoto Wao

Watoto wawili katika familia moja walikuwa wanapata kipigo kikali kutoka kwa baba yao. Siku moja baada ya kupata cha mtema kuni, waliandika maneno haya kwenye chumba cha kulala cha baba yao. ” Uwe na huruma kwa watoto wako nao watakuwa na huruma kwako, wako Mungu. ” Mtume Paulo wa Tarsus anawaasa wazazi, “msiwachokoze watoto wenu, …

Epuka Kitu Hiki Kwenye Malezi Ya Watoto

Watoto ni zawadi kutoka kwa Mungu. Watoto ni matunda ya ndoa. Watoto wenye maadili mazuri huwa wanatokea familia zenye maadili mazuri. Watoto wanakua bora pale ambapo wazazi wanakuwa bora. Shabaha yetu kubwa ya leo ni mzazi au mlezi kuepuka kuwalinganisha watoto. Usiwalinganishe watoto wako kwa sababu utakosa kujua upekee wao. Watoto huwa hawafanani hata siku …

Hii Ndiyo Hadithi Bora Ya Kuwafundisha Watoto Wako

Mpendwa rafiki yangu, Kumekuwa na mabadiliko makubwa sana katika zama tunazoishi, zama za mapinduzi ya viwanda kazi za kuajiriwa zilikuwa ni nyingi ukilinganisha na sasa.   Zama za taarifa zimekuwa na mabadiliko sana, binadamu yuko huru kufanya kile anachotaka yeye. Dunia inazidi kudhihirisha ukweli kwamba ile hadithi ya nenda shule, soma kwa bidii, faulu na …

Jinsi Ya Kumwamasisha Mtoto Wako Ili Aweze Kufaulu Sana Darasani

Rafiki yangu mpendwa, Sisi binadamu huwa tuna vitu viwili ambavyo vinatuhamasisha kuchukua hatua, kitu cha kwanza ambacho kinatuhamasisha kuchukua haraka ni kwa ya kupata furaha au raha na kingine kinachotuhamaisha kuchukua hatua ni kuepuka maumivu. Ziko hamasa za aina mbili zinazofanya kazi vizuri ambazo ukizitumia utaweza kumwamasisha mtoto wako na kufanya vizuri shuleni. Kila mzazi …

Hawa Ndiyo Watu Ambao Hupaswi Kuwakasirikia

Rafiki, Kukasirika ni asili ya binadamu, hatuwezi kuzuia kutokuwa na hisia za hasira bali tunaweza kuzikabilia au kuzitawala hisia zetu ili tusiweze kufanya mambo ya ajabu. Wote tunajua kuwa tunapokuwa na hisia za hasira huwa fikra zinakuwa chini yaani uwezo wa kufikiri unakuwa mdogo sana hisia zinakuwa juu. Ikitokea mtu mzima amekuja na kukufanyia kitu …

Hii Ndiyo Aina Ya  Upendo Ambao Wazazi Wanapaswa  Kuonesha Kwa Watoto Wao

Ukienda dukani kununua simu, pasi, TV unanunua kile kitu ukiwa umepewa namna ya  kukitumia kile kitu,ndani ya bidhaa utakuta kuna karatasi ya maelekezo. Hivyo basi, mtoto anapozaliwa hospitali hakuna kitabu cha maelekezo ambacho utapewa namna ya kumlea mtoto. Wengi wanajikuta wanawalea watoto kadiri ya wao walivyolelewa. Watoto mara nyingi wanapenda kujifunza kutoka kwa wazazi wao …

Kama Unataka Usipoteze Siku Yako Fanya Kitu Hiki

Rafiki, Kwa zama hizi za taarifa watu wamekuwa ni mabingwa wa kupoteza siku zao. Watu wako bize lakini hakuna kikubwa wanachoingiza wazungu wanasema busy for nothing. Changamoto ya zama hizi ni kwamba mitandao ya kijamii inawachangia sana kuwavuta watu kuvunja siku zao. Siku moja nilikuwa na mwadhiri wa chuo kikuu fulani, akaniambia yaani nikiamka nikishika …

Hii Ndiyo Lugha Bora Ya Kufundishia Watoto

Rafiki, Kila mmoja wetu alikuwa mtoto, kama unasoma hapa huenda una mtoto au unatarajia kupata mtoto. Watoto ni zawadi kutoka kwa Mungu, hivyo tunatakiwa kujifunza namna ya kuwalea watoto hawa ambao tumepewa kama zawadi. Wazazi wengi wanajua kuzaa lakini kwenye malezi kuna ubinafsi mkubwa. Unaweza kukuta mzazi anajijali yeye lakini ukienda kumuangalia mtoto wake, hawafanani …