Design a site like this with WordPress.com
Get started

Jinsi Ya Kuepuka Kujitengenezea Balaa

Vitu vingi katika maisha yetu, huwa tunavitengeneza sisi wenyewe, kwa mfano, tunatengeneza tabia na kisha tabia zinatutengeneza.

Hata wakati mwingine, balaa huwa mtu anajitengenezea, utaweza kushangaa sasa inakuwaje mtu anajitengenezea.

Kuna msemo mwingine unasema akili isiyoshughulika inakuwa ni karakana ya shetani. Mtu ambaye ameamka asubuhi na akaupangilia muda wa vizuri, hata shetani ni ngumu kumjaribu lakini mtu ambaye ana muda mwingi na hajapangilia siku yake ni rahisi kujaribiwa na shetani.

Aliyekuwa mbabe wa kivita na jemedari wa kijeshi Napoleon Bonaparte aliwahi kunukuliwa akisema, kila saa unayopoteza ni fursa ya kuwa na balaa hapo baadaye.

Kumbe basi, unajitengenezea balaa wewe mwenyewe kwa kila saa unayopitia bure. Ukiwa unafanya kazi ni ngumu kuanguka kwenye dhambi lakini yule mtu ambaye hana cha kufanya akili yake huwa inafikiri kutenda mambo mabaya.

Usipoteze muda wako kwani unapopoteza unakuwa unakaribisha fursa na balaa hapo baadaye.

Ipangilie siku yako vizuri sana, hata shetani akiiona atakuwa hana muda wa kukupata bali atakuogopa.

Kuwa na muda mwingi bila kuwa na kitu cha kufanya ni chanzo kibaya cha maovu.

Usipoteze muda, ukipoteza muda na muda utakupoteza aliwahi kusema Fr Faustin Kamugisha.

Hata wale watu ambao wanafanya makubwa ni wale ambao hawana muda mwingi, wale ambao wana muda mwingi ndiyo ambao hawana makubwa wanayofanya.

Njia ya uhakika ya kuchelewa ni kuwa na muda mwingi aliwahi kusema Leo Kennedy.

Hatua ya kuchukua leo; Linda na tumia muda wako vizuri ili usikaribishe balaa hapo baadaye.

Kumbuka, kila saa unayopoteza ni fursa ya kuwa na balaa hapo baadaye. Tumia muda wako vizuri, utajiepusha na mambo mengi sana.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505//0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: