Design a site like this with WordPress.com
Get started

Kila Mtu Anakwenda Kujua Jina Langu

Maisha bila hamasa hayawezi kwenda vizuri sana. Kwa sababu sisi ni binadamu tunapaswa kupata hamasa ili tuweze kujisukuma kufanya kile tunachopaswa kufanya bila kukata tamaa.

Kwa kuwa mimi ni Muuza Hamasa, Afisa Mhamasishaji Mkuu CIO (Chief Inspiration Officer na kwenda kukuuzia hamasa ambayo itafanya kila mtu ajue jina lako kupitia kile unachofanya.

Kwenye maisha kila mtu ana kitu ambacho akifanya huwa kina mpa hamasa, kwa sababu safari ya mafanikio makubwa ni ngumu mno, kuna kila aina ya changamoto hivyo bila kuwa na hamasa ya kufanya unafikiri nani atakwenda kukua jina lako?

Kuwa na kitu ambacho kinakupa hamasa kila siku, kuwa na mstari kutoka kwenye vitabu vya dini kama Biblia au Kuruani, ambao mstari huo ukiusimamia unapata hamasa lakini pia unapata kile unachotaka. Kwa mfano, uko mstari mmoja kwenye kitabu cha mwanzo, kama una sali na hupati kile unachoomba, unaweza ukamwambia Mungu sikuachi mpaka unibariki, kama watu wa kale waliweza kutumia mstari huo na kufanikiwa na wakabarikiwa wewe ni nani?

Nyimbo, Kama una nyimbo ambayo ukiisikiliza moyo wako unasuuzika sikiliza kila siku. Ukiisikiliza inakupa hamasa ya kupambana. Kwa mfano, mimi nina nyimbo ambazo nikizisikiliza napata hamasa kweli, kwenye eneo la kiroho, kiakili na mwili kwa mfano leo asubuhi nilikuwa nasikiliza wimbo unaoitwa kila mtu anakwenda kujua jina langu, wimbo umeimbwa na Watt White na unakwenda kwa jina la You’re Gonna Know My Name utafute utakupa hamasa sana lakini najua na wewe una nyimbo zako pia.

Kwenye kila eneo la maisha yako uwe na kitu cha kusimamia, tafuta hata nyimbo ambayo inakupa uamsho wa kiroho pale unapoisikiliza.

Ung’ang’anizi kwenye kile unachofanya kinakwenda kukufanya kila mtu ajue jina lako. Weka ung’ang’anizi, utafanikiwa kupata kile unachotaka.

Fanya kazi kweli, ili kila mtu aende kujua jina lako. Fanya vizuri sana kiasi kwamba hakuna mtu anayeweza kufanya kama wewe kwenye kile unachofanya. Kitu kikipita kwenye mkono wako, basi kifanye kwa ubora wa hali ya juu, fanya vizuri sana na ujiulize hivi navyofanya watu wote watakwenda kujua jina langu?

Hatua ya kuchukua leo; Na kila mtu aende kujua jina lako kupitia kazi, biashara au kile unachofanya. Kuwa mtu bora kwenye kile unachofanya na kila mtu atakwenda kujua jina lako kwa sababu ya kazi nzuri unayofanya.

Jipe changamoto, je, kwa jinsi unavyofanya kazi kila mtu atakwenda kujua jina lako kupitia kazi, biashara au huduma unayotoa?

Kwahiyo, jiambie kwamba “kila mtu anakwenda kujua jina langu kupitia kile nachofanya, na nitafanya mambo chanya tu, nitatoa thamani kubwa kwa wengine ili kila mtu aweze kujua jina langu. “

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505//0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: