Design a site like this with WordPress.com
Get started

Ifanye Siku Ya Mwenzako Kuwa Bora Kupitia Hiki Hapa

Huwezi kuishiwa pale unapotoa thamani kubwa kwa wengine. Kwa mfano, watu wanakula samaki kila siku lakini ulishawahi kusikia samaki wameisha baharini?

Ifanye siku ya mwenzako kuwa bora kupitia kile unachofanya.
Kile unachofanya kina msaidia mwenzako kuwa bora kwa namna moja au nyingine.

Kuna watu wanakutegemea kupitia kile ambacho, hata kama huoni mrejesho wake, lakini jua kuna watu wanakutegemea kupitia kile unachofanya, hivyo basi, wafanye wenzako wawe bora sana kupitia wewe.

Uwe daraja kwa WENGINE, unapojua kitu hakikisha kile unachojua kina kuwa msaada kwa wengine. Wewe fanya kwa sababu ni wajibu wako kufanya, siyo kila mtu atakuja kukushukuru kwa kile unachofanya, bali sababu ya kusaidia wengine itoke ndani yako bila msukumo kutoka nje.

Kama unafanya biashara au kazi wasaidie wateja wako kutatua changamoto zinazowakabili kwa kufanya hivyo unakuwa unafanya siku ya mwingine kuwa bora.

Unaposhindwa kutimiza wajibu wako, unakuwa unafanya siku ya mwingine kuwa mbaya. Hivyo basi, timiza wajibu wako ili watu wengine waweze kuwa bora.

Hatua ya kuchukua leo; Nenda kaifanye siku ya main kuwa bora kupitia kile unachofanya.

Nenda katoe huduma bora, nenda kawasaidie watu na watu wakikutana na wewe wapone maumivu yao na siyo kugeuka kuwa mwiba tena. Shabaha yako kuwa leo ni kwenda kufanya maisha ya wengine kuwa bora leo kupitia kile unachofanya.

Kila mtu anamwitaji mwingine ili aweze kufanikiwa, je, wewe watu wanakuhitaji kwa huduma gani leo? Umejiandaa kwenda kutoa huduma gani leo?

Kwahiyo, wawezeshe wengine kuwa bora kupitia kile unachofanya na asili itakulipa kwa kila zuri unalowafanyia wengine.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505//0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: